![]() |
|
Edward
Lowassa na alipochukua fomu ya kuwania urais kupitia Chadema.
Mjumbe mmoja wa
Kamati Kuu (CC) ya chama hicho, aliyeomba hifadhi ya jina lake, ameliambia
gazeti hili kuwa, madai yanayotolewa na watu mitaani na katika mitandao ya
kijamii yakisema Dk. Slaa amekasirishwa na kitendo hicho ni ya uongo.
ALIANZA
DK. SLAA, MBOWE MH!
Mjumbe huyo
alisema kuwa, Dk. Slaa ndiye mtu wa kwanza ndani ya Chadema kutoa wazo na
hatimaye kushiriki kikamilifu katika vikao vya kumwezesha Lowassa kujiunga na
chama hicho.
“Kwa taarifa yako,
Dk. Slaa ndiye aliyemtaka Lowassa ajiunge Chadema. Mbowe (Freeman, Mwenyekiti
wa Taifa Chadema) hakumtaka kabisa huyu jamaa aje kwetu. Kwa sababu hakuona
jinsi gani wangewaeleza wananchi juu yake, lakini mzee ndiye aliyeshawishi na
vikao vya kumjadili vikaanza mfululizo. Ukiangalia picha za awali, Dk. Slaa
yupo.”
MTOA
HABARI ASHIRIKI VIKAO
“Mimi
ninayekwambia ni Mjumbe wa Kamati Kuu, nimeshiriki zaidi ya vikao 14
vilivyokuwa vikimjadili Lowassa na vyote hivyo, Dk. Slaa alikuwepo. Huyu jamaa
hajakaribishwa kwa utashi wa mtu mmoja kama mnavyosikia huko nje na wala mzee
Mtei (Edwin, mwasisi wa chama hicho) hahusiki na chochote,” alisema mjumbe
huyo.
WABUNGE
WAKOROFI WALIAFIKI
Kwa mujibu wa
mjumbe huyo, ili kuondoa dhana kuwa, Lowassa anapelekwa Chadema na uongozi,
wabunge wote ‘wakorofi’ ndani ya chama hicho walikaribishwa kushiriki vikao 14
vya kumjadili ili pia wamuulize maswali na yapate majibu kitu ambacho
kilifanyika kwa ufanisi wa hali ya juu.
Aliwataja baadhi
ya wabunge hao ‘wakorofi’ na majimbo yao kwenye mabano kuwa ni pamoja na
Godbless Lema (Arusha Mjini), John Mnyika (Ubungo), Tundu Lissu (Singida
Mashariki), Joseph Mbilinyi (Mbeya Mjini), Halima Mdee (Kawe), Peter Msigwa
(Iringa Mjini), Joshua Nassari (Arumeru), Ezekiel Wenje (Nyamagana),
David Silinde (Mbozi Magharibi) na Highness Kiwia (Ilemela).
“Unajua, kwa
vyovyote vile, vikao kama vingefanywa na viongozi wa juu peke yao, hawa wabunge
wakorofi wangesumbua sana, lakini wote walishiriki na hakuna ambacho hawakijui.
Ndiyo maana wote wamekaa kimya kwa sababu taratibu zote zilifuatwa,” alisema
mjumbe huyo.
UKWELI
ULIVYO
“Hapa lazima
nikueleze ukweli. Kinachotokea kwa Dk. Slaa ni shinikizo kutoka familia yake.
Kuna watu walikuwa na matumaini makubwa ya kufaidika endapo yeye angegombea
tena na kushinda urais mwaka huu, hivyo wameamua kununa kwa sababu kilichotokea
hakina masilahi kwa familia.
YADAIWA
DK. SLAA ALITAKIWA KUCHAGUA MOJA
Mjumbe huyo
alikwenda mbali kwa kusema kuwa, wakati wa mchakato wa Dk. Slaa kutaka Lowassa
aingie Chadema baada ya kukatwa jina na Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)
mjini Dodoma, hakuiambia familia yake mpaka dakika za mwisho, ikajulikana.
“Ndipo familia
ikamweka chini na kumwambia achague moja. Aendelee na siasa za Chadema au
aachane na siasa hizo ili aangalie familia yake kwani kitendo chake
cha kuwa mstari wa mbele kumtaka Lowassa kiliashiria kuwa, yeye hatagombea tena
urais hivyo kuua matumaini ya familia. Ndiyo maana yupo kimya na hafiki
ofisini.”
CHADEMA
YAPANGA SAFU YA KUMSHAWISHI
“Sasa dokta ni mtu
mzima. Hawezi kuliamua hilo kirahisi kama unavyofikiria. Ni lazima aende nalo
taratibu ili kuziridhisha pande zote mbili. Na kwa kutambua hilo, chama
kimeunda jopo la watu, wakiwemo mapadri, mashehe na marafiki zake ili
wamshawishi arejee Chadema lakini akiiweka familia yake katika kuridhia na
kumwelewa,” alisema mjumbe huyo wa Kamati Kuu.
LOWASSA
AANIKA UKWELI KUHUSU RICHMOND
Kuhusu madai ya
muda mrefu ya chama hicho yanayomtaja Lowassa kuwa ni fisadi, mjumbe huyo
alisema kiongozi huyo aliwaeleza kwa ufasaha kuhusu utajiri wake na
wakaridhika. Kwa upande wa Richmond, aliwaeleza kuwa alishataka kuuvunja
mkataba huo, lakini mamlaka ya juu ikamzuia.
TAASISI
TOKA NJE YATUA NCHINI KUTAFITI
Juu ya nafasi yao
kushinda urais wakiwa na Lowassa, mjumbe huyo alisema kabla ya kuafiki
kumtangaza kugombea, kwa gharama za Chadema, walikodi taasisi ya utafiti kutoka
nchini Ujerumani kuja Tanzania ili kufanya utafiti nchi nzima kama Lowassa
anakubalika.
Alisema utafiti
ulipokamilika, ikaonesha kuwa, kama uchaguzi mkuu ungefanyika Julai 2015,
Lowassa alikuwa mbele ya wagombea wenzake kwa asilimia 65.
SLAA
KIMYAAA!
Hadi gazeti hili
linakwenda mtamboni, Dk. Slaa hajajitokeza kuelezea kilichosababisha ukimya
wake huku akiwa hapokei simu ya Uwazi kitu kinachozidisha kwa kasi maneno
mitandaoni juu ya hatima yake ndani ya chama hicho kikuu cha upinzani.
Alhamisi iliyopita
gazeti dada na hili, Uwazi Mizengwe linalotoka kila Ijumaa, waandishi wake
walishinda nyumbani kwa Dk. Slaa, Mbweni nje kidogo ya Jiji la Dar lakini
walishindwa kuongea naye licha ya kumpelekea karatasi yenye ujumbe wa kumuomba
kuzungumza naye, waliambulia kumuona kwa mbali akiwa ndani ya geti la nyumba
yake.
Source:-Global Publisher's.
Pata
Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori
inayonifikia wakati wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
Tuesday, August 04, 2015
KUHUSU DK. SLAA KUMKATAA LOWASSA:- Ukweli ni Huu...Hapa soma..
Tags
# SIASA
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
SIASA
Labels:
SIASA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.







Huna haya hata kdg, kama huna cha kusema kaa kimya
ReplyDelete