Wagombea wa UKAWA na Mwenyekiti wa
UKAWA wakionyesha Kitabu chao cha Ilani ya Uchaguzi mwaka 2015.
ARDHI, MAJI NA KILIMO
1.
Tutaimarisha mfumo wa umiliki wa
ardhi kwa Watanzania na kudhibiti migogoro ya ardhi hasa kati ya wakulima na
wafugaji.
2.
Tutapima ardhi yote ya Tanzania na
kumilikisha vijiji na wakulima kwa hati za serikali ili kuipa thamani.
3.
Tutaleta mapinduzi ya kilimo kwa
kuimarisha elimu, ufundi na teknolojia ya kisasa na kumkomboa mkulima kutoka
jembe la mkono.
4.
Tutasimamia kilimo, ufugaji na uvuvi
wa kisasa na kuunganisha sekta hizo na ya viwanda.
5.
Kuhakikisha kuwa wananchi wanatunza
na kulinda vyanzo vya maji.
6.
Tutakuza kilimo cha umwagiliaji kwa
kuwapa wakulima elimu na mikopo ya riba nafuu ya kuvuna maji na kujenga
miundombinu husika.
7.
Tutaweka mazingira rafiki
yatakayomhakikishia kwa kila Mtanzania kupata maji safi na salama. Kumaliza
kero za maji nchini kutamkomboa mwanamke kutokana na adha ya kuchota maji kwa
kichwa.
8.
Nitafuta kodi zote za mazao na
mifugo kwa wakulima na wafugaji.
9.
Tutasimamia kilimo cha biashara
kinachozingatia maslahi ya nchi na ya Watanzania.
10.
Tutaanzisha programu maalum ya
kufufua mazao asilia ya Tanzania hususan mkonge.
11.
Tutaanzisha Benki ya Maendelo ya
Ufugaji na Uvuvi.
MIUNDOMBINU
1.
Tutaboresha bandari zilizopo na kujenga
mpya kama vitega uchumi vya Taifa ili kurejesha biashara tulizopoteza kwa
bandari za nchi jirani.
2.
Tutajenga barabara nchini kwa
kuzingatia ubora hasa zile za vijijini.
3.
Tutajenga reli ya kati kwa viwango
vya kisasa
4.
Tutajenga shirika la Ndege la Taifa
linalojiendesha kwa misingi ya faida.
5.
Tutajenga miundombinu ya kisasa na
kuondosha misongamano ya magari hasa katika majiji ya Dar es salaam, Mwanza,
Mbeya na Arusha
6.
Tutaimarisha uzalishaji na
usambazaji wa umeme vijijini ili kufikia zaidi ya asili mia sabini na tano ya
Watanzania
VIWANDA
1.
Tutaimarisha sekta ya viwanda kuwa
mhimili wa uchumi kwa uzalishaji wa bidhaa na ajira endelevu
2.
Tutajenga viwanda vipya vya
kusindika mazao ya kilimo, uvuvi na ufugaji.
3.
Tutahakikisha kuwa ndani ya miaka
mitano mali ghafi zote za Tanzania zinasindikwa kabla ya kusafirishwa nje ili
kuongeza mapato na ajira ya mamilioni ya vijana.
4.
Tutaanzisha Benki ya Ukuzaji wa
Viwanda
UCHUMI
1.
Tutabadili mfumo wa Uchumi wa nchi
ili kuhakikisha kuwa mfumo wa uchumi wa Tanzania unakuwa ni wa soko-kijamii
ambapo nguvu za soko zitatumikia jamii kwa serikali kuweka uwiano wa mapato
unaohakikisha huduma za kijamii zinapatikana kwa ufanisi.
2.
Tutalinda sekta binafsi na bidhaa za
ndani kwa kuwapa Watanzania upendeleo wa maksudi kwa kipindi cha mpito ili
waimarike na waweze kuhimili ushindani.
Tutawapa wafanyabiashara wetu upendeleo
katika manunuzi ya serikali na kuwajengea mazingira mazuri ya biashara na kodi
endelevu.
3.
Tutawawezesha Watanzania kupata
mitaji ya biashara kwa masharti nafuu kabisa.
4.
Tutavutia uwekezaji na wawekezaji
wenye tija. Kuweka udhibiti wa wahamiaji wasioleta tija wala maslahi kwa Taifa.
5.
Tutaimarisha sera ya ubia baina ya
Serikali na Sekta binafsi kwenye maeneo muhimu ya kiuchumi na kibiashara. Pia,
kuwawezesha Watanzania kuwekeza kwa njia ya ubia na wawekezaji wenye mitaji
mikubwa bila kujali wanapotoka.
6.
Tutaimarisha usimamizi kwa
kubadilisha mfumo wa Vyama vya Ushirika nchini ili utokane na uendeshwe na
wakulima wenyewe ikiwa na pamoja na kuwawezesha kuboresha makazi kwa mpango wa
kushirikiana kujenga nyumba bora
7.
Tutaanzisha na kuwezesha uanzishaji
wa viwanda vidogovidogo vinavyotoa ajira kwa wingi kwa kuvihusisha na vyuo vya
ufundi na benki maalum kwa lengo hilo.
AJIRA
1.
Tutasimamia swala la ajira hasa kwa
vijana kwa kukuza elimu ya ufundi ili waweze kujiajiri
2.
Tutazipa kipaumbele sekta
zinazozalisha ajira kwa wingi hasa za viwanda, kilimo, ufugaji, uvuvi na utalii
na kuzipa unafuu wa kodi ili zikue kwa haraka.
3.
Tutawapa wawekezaji wakubwa katika
sekta hizi upendeleo maalum na viwango vya kodi nafuu.
NISHATI NA MADINI
1.
Serikali itashiriki kikamilifu
katika uzalishaji wa nishati
2.
Itatengeneza mazingara mazuri ya
kisera yatakayovutia na kuwezesha ushiriki wa Watanzania na ubia kati yao na
wageni.
3.
Serikali yangu itaupa uzalishaji
mkubwa wa umeme wa maji kipaumbele namba moja, umeme wa makaa ya mawe
kipaumbele namba mbili, umeme wa gesi asilia kipaumbele namba tatu na umeme wa
urana kipaumbele namba nne.
4.
Serikali itatoa vipaumbele muhimu
kwenye usambazaji wa huduma kubwa ya umeme sehemu za uzalishaji uliyolenga
masoko ya ndani, ya nchi jirani na ya nchi za kigeni.
5.
Itapitia upya mikataba yote mikubwa
ya nishati na madini ili kubaini iliyo mibovu na kuifanyia maboresho.
6.
Serikali yangu itatumia sehemu ya
hisa zake kwenye raslimali kubwa ya gesi asilia iliyopatikana hapa nchini kama
rehani kwenye kujichukulia mikopo kwa ajili ya ujenzi wa miundo mbinu ya
mabomba ya gesi.
7.
Serikali itatoza kodi na ada ndogo
zaidi kwa wazawa wenye ubia kati yao na wageni kuliko zitakazotozwa kwa wageni
wasiowekeza kwa kushirikisha wazawa.
8.
Serikali itasitisha utoaji wa
misamaha ya kodi isiyo lazima kwenye sekta ya madini, na badala yake itawekeza
kwenye kuongeza thamani ya raslimali zake za madini.
9.
Tutakuza nishati mbadala kutamkomboa
mwanamke kutokana na adha ya kukata kuni
MALIASILI NA UTALII
1.
Tutasimamia uvunaji na matumizi ya
rasilimali za Taifa kwa manufaa ya kila Mtanzania wa kizazi hiki na kijacho
2.
Tutapiga vita ujangiri na kuimarisha
utunzanji wa hifadhi za taifa na mazingira
3.
Tutachochea ujenzi wa miundombinu ya
utalii nchini ikiwa ni pamoja na ujenzi wa mahoteli na kuimarisha mafunzo
4.
Tutaongeza idadi ya watalii kufikia
milion mbili ifikapo 2020
UTAWALA BORA, ULINZI WA NCHI NA
USALAMA WA RAIA
1.
Tutasimamia Katiba mpya inayolinda haki
za msingi za wananchi na kuweka bayana mipaka ya madaraka ya serikali na
viongozi, Bunge na Mahakama.
2.
Tutaboresha miundobinu ya sheria na
kuimarisha utendaji wa Mahakama na maslahi ya wafanyakazi
3.
Tutasimamia haki za raia na
kuangalia upya sheria kandamizi ili wananchi kama Masheik wa Zanzibar hawasoti
jela kwa sababu za kisiasa.
4.
Tutaimarisha mafunzo ya vyombo ya
Polisi hasa wapelelezi na waongoza mashtaka ili wapate uwezo wa kusimamia
utoaji wa haki.
5.
Tutavipa vyombo vyote vya ulinzi na
usalama nyenzo na kuboresha mazingira yao ya kazi na maslahi
UZALENDO, UTENDAJI NA UWAJIBIKAJI
1.
Tutajenga uzalendo ili kila
Mtanzania aweze kutathmini mchango wake kwa taifa kila siku
2.
Tutaimarisha nidhamu, utendaji na
uwajibikaji katika Sekta ya Umma
3.
Tutaimarisha mchango wa Wataalam
wetu, wanawake na vijana katika kusimamia uchumi na kuwajengea mazingira
stahiki ya kazi pamoja na mafao.
4.
Tutapiga vita rushwa na ubadhirifu
katika sekta ya Umma na binafsi
5.
Tutadhibiti na kupunguza matumizi ya
serikali ikiwa ni pamoja na kufuta safari za watumishi serikalini zisizokuwa
muhimu pamoja na zile za Rais na kupiga marufuku matumizi ya mashangingi
serikalini.
6.
Tutadhibiti deni la Taifa kwa kuanza
na ukaguzi wa madeni ya serikali ili kuhakiki jinsi yalivyotumika
7.
Tutaimarisha uwazi na kuondoa usiri
katika shughuli za serikali na kuweka bayana mikataba yote ya nchi ikiwa ni
pamoja na ile ya mafuta, madini na gesi asilia
KUKUZA PATO LA SERIKALI
1.
Tutadhibiti mapato kutokana na
raslimali kwa kupitia upya viwango vya mirabaha kutokana na madini na gesi
asilia ili kuhakikisha kuwa Tanzania inapata gawio stahiki.
2.
Serikali itaanzisha Wizara maalum
itakayosimamia nishati ya gesi na mafuta.
3.
Tutaimarisha ofisi ya Msajili wa
Hazina ili kusimamia vema uwekezaji wa Serikali katika mashirika na mapato
yake.
4.
Tutahakikisha kuwa mashirika ya umma
yanaendeshwa kwa misingi ya faida na uadilifu.
5.
Tutadhibiti ukwepaji kodi za ushuru
wa forodha na kupiga marufuku misamaha ya kodi holela ili kuokoa mabilioni ya
fedha yanayopotea kila wiki.
6.
Sambamba na hilo tutarahisisha
utaratibu wa kulipa kodi ili kuondoa kero na mazingira ya rushwa. Kwa kudhibiti
makusanyo ya kodi tutakusanya fedha za kugharimia huduma za msingi kama afya na
elimu kikamilifu.
KUIMARISHA MUUNGANO
1.
Tutaimarisha umoja, usalama na udugu
wa Watanzania na Muungano kwa misingi ya haki na usawa.
WANAWAKE, WATOTO NA WAZEE
1.
Wanawake watapewa fursa na haki sawa
katika elimu na uchumi ili waweze bila kuwezeshwa.
2.
Tutahakikisha wazazi wanapata fursa
ya kuwa walezi na wafanyakazi kwa kuongeza urefu wa likizo ya uzazi
3.
Tutaimarisha elimu ya watoto hasa
wasichana na kukuza fursa zao na kukomesha ndoa za watoto wadogo.
4.
Tutaongeza uwakilishi wa akina mama
katika ngazi zote serikalini na mashirika yake kufikia asili mia hamsini
ifikapo 2020.
5.
Wazee na wasiojiweza watapewa posho
ya kujikimu inayokidhi mahitaji ya msingi itakayowawezesha kuishi kwa heshima
na kulinda utu wao ndani ya familia na jamii zao.
SANAA, UTAMADUNI NA MICHEZO
1.
Tutaendeleza na kuwezesha vipaji vya
sanaa na michezo
2.
Tutarudisha viwanja vya michezo
vilivyovamiwa
3.
Tutafuta kodi zote za vifaa vya
michezo.
4.
Tutadhibiti viwango na maadili ya
bidhaa za nje zinazoingizwa nchini na kuzitoza kodi halisia
5.
Tutajenga taasisi na vyuo vya kukuza
michezo ili kuhakikisha kuwa ndani ya miaka mitano Tanzania inashiriki kwa
ushindi katika mashindano ya kimataifa ya soka na riadha
6.
Tutalinda Hakimiliki za sanaa nchini
7. Tutafuta kodi za sanaa kwa wasanii chipukizi ili kuwapa muda kwa kujijenga.
SERA YA MAMBO YA NJE YENYE TIJA KWA
TAIFA
1.
Tutakuza ushirikiano wa Kimataifa
wenye tija na Ujirani mwema.
2.
Tutatetea haki za binadamu, usawa wa
nchi na kuimarisha ushiriki wa Tanzania katika diplomasia ya kimataifa.
3.
Tutakuza umoja na ushirikiano wa
Umoja wa Afrika, Jumuia ya Afrika Mashariki, SADC na Umoja wa Mataifa.
4.
Tutaimarisha Umoja wa Mataifa ikiwa
ni pamoja na kudai mabadiliko ya mfumo ili kuleta usawa wa nchi shiriki.
Ndugu Watanzania
Naomba nimalizie kwa kusema
yafuatayo
1.
Natambua kuwa uongozi ni dhamana.
Mkinichagua nitaienzi dhamana hiyo kwa utendaji uliotukuka.
2.
Nawaahidi Watanzania kuwa kwa uwezo,
akili, uzoefu na nguvu zangu zote nitawatumikia. Nawaomba nanyi mniahidi jasho
lenu na uwezo wenu wote ili kwa pamoja tuvuke. Tutajikomboa toka utawala wa CCM
unaodumaza uchumi na maendeleo. Tutaanza safari ya uhakika kuondoa umaskini.
3.
Mabadiliko pia ni kuthamini utu na
kukataa hadaa ya hongo ili kuuza haki yako ya kuchagua. Msikubali rubuni za
uchaguzi kwa kupewa pesa au vitu. Rushwa ya uchaguzi ndiyo sera ya CCM.
Ukikubali basi umeuza pia haki na sauti yako ya kuwalalamikia walio madarakani.
Imetosha. Tukatae. Tulinde utu na haki zetu. Tuchague mabadiliko.
4.
Mabadiliko ni fikra. Ni kufikiri na
kutenda tofauti. Hatuwezi kuendelea kufikiri na kutenda kama kwamba hatuna
dharura ya maendeleo. Kwanza tuanze kwa kufanya mabadiliko na tujiamini kuwa
sisi kama Taifa tunaweza.
Tunaweza kujitegemea na kuleta maendeleo yetu wenyewe
bila kutegemea wafadhili. Hii si ndoto. Nchi nyingi zimefanikiwa kuondoa
umaskini katika kizazi kimoja. Tujifunze kutoka kwao.
5.
Tuwe taifa linalotumia raslimali
zake kujiendeleza na siyo kuwanufaisha wageni na kuwafanya Watanzania watwana
katika nchi yao. Inabidi tuache kuwa taifa ombaomba. Tuache kuukubali na kuvaa
umaskini kama joho la fahari.
6.
Mabadiliko ya kweli hayawezi kuletwa
na CCM. Tusitegemee kuwa leo wana jipya. Ndiyo maana ahadi walizotoa miaka
thelathini iliyopita ndizo wametoa juzi. Tukatae hadaa. Miaka hamsini ya CCM
imetosha.
7.
Tunaamani kwamba tutashinda kwa
sababu Watanzania mpo nyuma yetu. Watanzania mmeamua kuleta mabadiliko. Kura
yako ndiyo itakayokuwa mkombozi wako. Hakikisha unapiga na kuilinda kura yako.
Wakati wa mabadiliko ni sasa.
Mungu ibariki Tanzania. Asanteni
sana.
PAPO KWA PAPO Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo
na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia
tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
Sunday, August 30, 2015
Home
HABARI
KAMPENI ZA UKAWA UCHAGUZI MKUU 2015:-Isome Hotuba ya Mgombea Edward Lowassa ya kuzindua Ilani.
KAMPENI ZA UKAWA UCHAGUZI MKUU 2015:-Isome Hotuba ya Mgombea Edward Lowassa ya kuzindua Ilani.
Tags
# HABARI
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
HABARI
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment