KAMPENI ZA UCHAGUZI MKUU 2015:-Taswira Picha ya Uzinduzi wa kampeni UKAWA ulivyofana August 29,2015. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, August 30, 2015

KAMPENI ZA UCHAGUZI MKUU 2015:-Taswira Picha ya Uzinduzi wa kampeni UKAWA ulivyofana August 29,2015.


Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa pamoja na Mgombea mwenza, Mh. Juma Duni Haji wakiwasili kwenye viwanja vya Jangwani Jijini Dar es salaam, kulikofanyika Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Chama hicho, Agosti 29, 2015.BOFYA HAPA KUISOMA HOTUBA YA Mh.LOWASSA.


PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.



Hii leo August 30,2015, Mh Edward Lowassa akiambatana na waziri mkuu mstaafu Mh Fredrick Sumaye wameanza kazi ya kunadi sera zao mikoani katika mkoa wa Iringa huku wakiendelea kuungwa mkono na maelfu ya wananchi na viongozi akiwemo aliyewahi kuwa waziri katika wizara mbalimbali mh Joseph Mungai.

Wakiwa mkoani Iringa kwenye mikutano iliyofanyika Mafinga wilayani Mufindi, Ilula wilayani kilolo na Iringa mjini wanasiasa hao pamoja na kunadi sera na kuwaombea kura wagombea wao wa ubunge na udiwani wameendelea  kuelezea athari zinazolikabili taifa zinazochangiwa na usimamizi na ubabe wa viongozi wa CCM na wamewataka watanzania kuendelea kuunganisha nguvu na kukiondoa madarakani sambamba na kuelezea azma yake ya dhati ya kufanya marekebisho makubwa na kwa wakati na kuzisimamia kikamilifu. 


Umati wa wakazi wa Jijini Dar es salaam, ukiwa umefurika kwa wingi kwenye viwanja vya Jangwani kuwalaki Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa pamoja na Mgombea mwenza, Mh. Juma Duni Haji, walipokuwa wakiwasili viwanjani hapo, kulikofanyika Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Chama hicho,  Agosti 29, 2015.


Wafuasi wa Vyama vinavyounda UKAWA wakiwashangilia Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa pamoja na Mgombea mwenza, Mh. Juma Duni Haji, walipokuwa wakiwasili viwanjani hapo, kulikofanyika Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Chama hicho,  Agosti 29, 2015.


Wafuasi wa Vyama vinavyounda UKAWA wakionyesha furaha yao kwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa.

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Mgombea Urais wa Zanzibar katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad wakati alipowasili kwenye viwanja vya Jangwani Jijini Dar es salaam, kulikofanyika Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Chama hicho,  Agosti 29, 2015.



Sehemu ya Wanahabari kutoka Vyombo mbali mbali nchini wakiendelea kuchukua habari za Mkutano huo, uliofanyika jioni ya Jumamosi kwenye viwanja vya Jangwani Jijini Dar es salaam na kuhudhulia na maelfu ya Wakazi wa jiji hilo.


Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe akimkabidhi, Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa pamoja na Mgombea mwenza, Mh. Juma Duni Haji, Kitabu cha Ilani ya Uchaguzi ya Chama hicho kwa mwaka 2015/2020 mara baada ya kuizindua, Jana Agosti 29, 2015.


Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, Mgombea mwenza, Mh. Juma Duni Haji pamoja na Mgombea Urais wa Zanzibar katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad wakionyesha vitabu cha Ilani ya Uchaguzi mara baada ya kuzinduliwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe.BOFYA HAPA KUISOMA HOTUBA YA Mh.LOWASSA.

Viongozi wa Vyama mbali mbali vinavyounda UKAWA wakionyesha Ilani hiyo mbele ya maelfu ya wakazi wa Jiji la Dar es salaam,  Agosti 29, 2015.


Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe (kulia) akiwatambulisha baadhi ya Wagombea Ubunge katika Majimbo mbali mbali ya jijini Dar es salaam.

Mwenyekiti Mwenza wa UKAWA, Mh. James Mbatia akizungumza kwenye Mkutano huo.

Watu wa Msalaba Mwekundu wakiwa wamembeba mmoja wa wakazi wa Jiji la Dar aliepoteza fahamu kwa kukosa hewa kutokana na uwingi wa watu uliofurika kwenye viwanja vya Jangwani, Jijini Dar es salaam  Agosti 29, 2015.

Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Fredrick Sumaye akitoa salamu zake kwa wakazi wa Jiji la Dar es salaam waliofurika kwenye viwanja vya Jangwani jijini Dar es salaam  Agosti 29, 2015.

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akiteta jambo na Mgombea Mwenza wake, Mh. Juma Duni Haji, wakati wa Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Chama hicho, uliofanyika  Agosti 29, 2015.

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akihutubia katika Mkutano huo wa Uzinduzi wa Kampeni za Chama hicho, uliofanyika  Agosti 29, 2015.

Mmoja wa wanasiasa wakongwe waliotoka CCM, Tambwe Hiza akisalimia.

PAPO KWA PAPO Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad