KAMPENI ZA UCHAGUZI MKUU 2015:- ACT wazalendo chazindua rasmi kampeni na kusisitiza kuimarisha uzalendo. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, August 30, 2015

KAMPENI ZA UCHAGUZI MKUU 2015:- ACT wazalendo chazindua rasmi kampeni na kusisitiza kuimarisha uzalendo.

Mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Anna Mghwira (kushoto), akihutubia katika uzinduzi wa kampeni ya chama hizo uliofanyika viwanja vya Zakhem Mbagala jijini Dar es Salaam leo August 30,2015.

Mgombea huyo wa Urais kwa tiketi ya ACT wazalendo Bi Anna Mghwira akihutubia katika mkutano huo, amesema iwapo atapata ridhaa ya kuiongeza serikali ya awamu na tano, ataunda serikali ya umoja wa kitaifa na kusimamia vipaumbe vinne vya chama hicho ikiwemo kila mwananchi kuwemo katika mfumo wa hifadhi ya jamii, mfumo shirikishi wenye kuzalisha ajira bora pamoja na afya.


Katika uzinduzi huo ,ACT wazalendo kupitia viongozi wake,Wamesitiza kitajikita katika kuimarisha uzalendo, kupambana na rushwa na ufisadi kwa kurejesha miiko ya uongozi ikiwemo kila kiongozi kuhorodhesha mali alizonazo na namna alivyozipata iwapo kitapata ridhaa. 


Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Kabwe Zitto akihutubia katika uzinduzi huo na kusema bila ya kurejesha miiko ya uongozi haitawezekana kupiga vita rushwa na ufisadi ambapo amepinga siasa zinazofanywa na baadhi ya vyama vya kutaka kukomesha ufisadi na rushwa kwa kutumia baadhi ya viongozi waliowasababishia wananchi shida na kadhia mbalimbali wanazozipata.
Mshauri wa Chama cha ACT-Wazalendo, Profesa Kitila Mkumbo akihutubia kwenye uzinduzi huo.
 
Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Kabwe Zitto (kushoto), akiteta jambo na  Mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Anna Mghwira.
Viongozi mbalimbali wa chama hicho wakiimba wimbo wa taifa. 
Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Kabwe Zitto, akiwatambulisha wagombea ubunge wa majimbo yote ya Dar es Salaam.
Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Kabwe Zitto, akigawa ilani ya chama hicho kwa mgombea urais na mwenza wake. 
Mgombea Mwenza, Hamad Mussa Yusuph akihutubia kwenye uzinduzi huo ambapo mara kukabidhiwa ilani ya chama cha ACT wazalendo, ameahidi kukomesha kero za watanzania na kuwataka kutumia kura zao katika kufanya mabadiliko badala ya kutumia nguvu na vurugu kama baadhi ya raia wa nchni nyingine duniani wanavyofanya.
Mwana muziki Bwana misosi, akitoa burudani katika uzinduzi wa kampeni wa Chama cha ACT-Wazalendo uliofanyika viwanja vya Zakhem Mbagala Dar es Salaam leo.
Umati wa Wananchi ukiwa katika uzinduzi wa kampeni wa Chama cha ACT-Wazalendo uliofanyika viwanja vya Zakhem Magala Dar es Salaam leo August 30,2015.

Chama cha ACT wazalendo ni chama cha pili cha siasa na cha kwanza kwa vyama vya upinzania kwa kusimamisha wagombea ubunge katika majimbo mengi zaidi ambapo kimeweza kusimamisha wagombea katika majimbo 219 kati ya majimbo 265 ya jamhuri ya muungano wa Tanzania na kikiongozwa na chama cha CCM kilichosimamisha wagombea katika majimbo yote 265 na chama cha demokrasia na maendeleo kimeshika nafsi ya tatu kwa kusimamisha wagombea katika majimbo.
 


(Picha zote kwa hisani ya :-mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062}

PAPO KWA PAPO Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad