Mgombea
mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu akiwa jukwaani akinadi ilani ya Chama Cha Mapinduzi
Jimbo la Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba. Na Joachim Mushi, Singida .
Mjumbe wa
Kamati ya Kampeni Taifa, Mwigulu Nchemba ambaye pia ni mgombea wa ubunge Jimbo
la Iramba Magharibi akizungumza na wananchi kuinadi ilani ya CCM.
Baadhi ya
wanaCCM na wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa Chama
Cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika katika Jimbo la Iramba Magharibi.
Mbunge
Nkenge CCM aliyemaliza muda wake, Asumpta Mshana akiinadi ilaya ya CCM.
Helkopta ya
mgombea ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini ikitua.
Mgombea
ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini anayeomba kuchaguliwa tena, Lazaro
Nyarandu akiwarudisha baadhi ya wananchi kurudi eneo la Mkutano wa kampeni na
kuacha kushangaa helkopta.
Mgombea
ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini anayeomba kuchaguliwa tena, Lazaro
Nyarandu akielekea eneo la mkutano pamoja na baadhi ya wananchi baada ya kutua
na helkopta.
Helkopta
iliyomshusha gombea ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini anayeomba kuchaguliwa
tena, Lazaro Nyarandu ikiwa inamsubiri.
Mjumbe wa
Kamati ya Kampeni Taifa, Mwigulu Nchemba (kushoto) wakimpongezana Katibu wa CCM
Mkoa, Merry Mziku jimboni Iramba Magharibi.
Bi. Suluhu
kulia akizungumza neno na Mwigulu Nchemba na Bi. Mziku.
Mjumbe
wa Kamati ya Kampeni Taifa, Mwigulu Nchemba ambaye pia ni mgombea wa ubunge
Jimbo la Iramba Magharibi akizungumza na wananchi kuinadi ilani ya CCM.
Baadhi ya
wanaCCM na wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa Chama
Cha Mapinduzi (CCM.
Mjumbe wa
Kamati ya Kampeni Taifa, Mwigulu Nchemba ambaye pia ni mgombea wa ubunge Jimbo
la Iramba Magharibi akizungumza na wananchi kuinadi ilani ya CCM.
Burudani
kidogo kabla ya ilani kuendelea kunadiwa jimboni Iramba.
Na Joachim Mushi, Singida .
MGOMBEA
ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini anayeomba kuchaguliwa tena, Lazaro
Nyarandu amenogesha kampeni za mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Bi.
Samia Suluhu katika mikutano yake inayoendelea ya kuinadi ilani ya CCM.
Nyarandu
ambaye jana August 29,2015 alishuka kwa helkopta ya kukodi Jimboni kwake ikiwa
ni muda mfupi baada ya mkutano wa kampeni kuanza alivuta hisia za wanaCCM na
wananchi katika mkutano huo. Kama hiyo haitoshi mgombea huyo wa ubunge alitumia
helkopta hiyo kwenye mikutano ya kampeni za mgombea mwenza ya Jimbo la Iramba
Magharibi.
Akihutubia
mkutano wa kampeni katika Kata ya Kengege, Jimbo la Iramba Magharibi mkoani
Singida, Bi. Suluhu aliwaomba wananchi kuipigia kura CCM kwani ndani ya ilani
yake imepanga kufanya mambo mazuri kwa maendeleo ya mkoa huo.
Alisema endapo watachanguliwa watajenga
kiwanda kikubwa cha kusafishia mafuta ya alizeti jambo ambalo litaongeza
thamani ya mazao kwa wakulima wa eneo hilo.
Aliongeza
kuwa mbali na kiwanda hicho kikubwa kuwanufaisha wakulima pia kitatoa nafasi za
ajira kwa vijana ambapo jumla ya wafanyakazi 600 watapata ajira ndani ya
kiwanda hicho, alisema baada ya Serikali ya awamu ya nne kujenga shule za
Sekondari za kata za kutosha na maabara ilani mpya ya CCM imepanga
kushughulikia suala la vifaa vya maabara hizo ili ziweze kutumika kwa ufasaha.
Bi. Suluhu
alisema Mkoani Singida imepanga kujenga hospitali kubwa ya rufaa ambayo itakuwa
ikitoa huduma katika mkoa huo na mikoa ya jirani, pamoja na ujenzi wa barabara
ya Ndago.
Aidha
akihutubia katika Mkutano mwingine Wilaya ya Ikungi aliahidi kufanya jitihada
za ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Ikungi ili kusongeza huduma kubwa za afya
kwa wanaIkungi, pamoja na kuvipatia umeme vijiji ambavyo bado havijafikiwa na
huduma hiyo kupitia mradi wa Wakala wa Umeme Vijijini (REA) awamu ya pili.
Aliongeza
kuwa licha ya maeneo ya mikoa ya singida kukabiliwa na tishio la ukame
aliwahakikishia hakuna raia atakayekufa njaa katika maeneo hayo.
"...Serikali imejipanga na ghala la kuhifadhi chakula lina akiba ya
kutosha, hivyo niwahakikishie hakuna mwanakijiji ambae atakufa kwa njaa.
Kwa upande
wake Mjumbe wa Kamati ya Kampeni Taifa, Mwigulu Nchemba ambaye pia ni mgombea
wa ubunge Jimbo la Iramba Magharibi akizungumza jimboni hapo alisema ilani ya
CCM imepanga kutekeleza miradi ya maji katika Vijiji vya Mgundu, Kinampanda,
Makunda pamoja na vijiji vingine vinavyokabiliwa na kero ya maji.
Alisema
baadha ya mradi wa ujenzi wa shule za Sekondari za kata kufanikiwa serikali
itakayoundwa na CCM imepanga kusimamia ujenzi wa mabweni ili kuwanusuru watoto
wanaotembea umbali urefu kwenda shuleni pamoja huku wasichana wakikabiliwa na
changamoto za kubebeshwa mimba na kukatishwa masomo yao.
Mwingulu
aliwataka wananchi kutochagua vyama vingine kwani havina hoja za msingi na
vingine vinaazima hadi wagombea ili viweze kuwasimamisha. Bi. Suluhu anaendelea
na ziara yake ambapo sasa anaelekea Mkoa wa Dodoma akiinadi ilani ya CCM.
PAPO KWA PAPO Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo
na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia
tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
No comments:
Post a Comment