Zitto Kabwe akihutubia wananchi katika moja
kati ya mikutano ya ACT - Wazalendo .
Chama cha ACT- Wazalendo kimepanga kuzindua
kampeni zake za uchaguzi Mkuu, Jumapili, Agosti 30,2015 maeneo ya Mbagala,
Temeke, jijini Dar es Salaam.
Taarifa za uzinduzi wa kampeni zilitolewa na
afisa habari wa chama hicho, Abdalah Khamisi ambaye alieleza kuwa chama hicho
kitaanza rasmi kuwanadi mgombea urais, Anna Mghwira na mgombea mwenza Hamad
Musa.
Kiongozi Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe
ambaye alikuwa mwanachama wa CHADEMA, anatarajiwa kuongoza kampeni hizo na kuwa
kivutio zaidi kutokana na historia yake nzuri ya kuvumbua ufisadi pamoja na
msimamo wake wa kuwatetea wananchi bungeni.
Mgombea urais wa ACT- Wazalendo, Bi. Anna
Mghwira ( Pichani ) atakabidhiwa sera za chama hicho baada ya kuteuliwa na chama chake
baada ya mmoja kati ya waasisi wa chama hicho, Profesa Kitila Mkumbo kukataa
kugombea nafasi hiyo licha ya kuchukuliwa fomu katika ofisi za Tume ya Taifa.
Mgombea wa
UKAWA pichani, Bw.Edward Lowassa akiwa katika ziara zake kbla ya kuzindua kampeni
Jumamosi August 29,2015.
Chama hicho
kitakuwa chama cha tatu kuzindua rasmi kampeni zake baada ya CCM iliyozindua
Jumapili ya August 23, 2015 iliyopita na CHADEMA chini ya mwamvuli wa UKAWA
wanaopanga kufanya uzinduzi Jumamoji hii ya August 29, 2015 kwenye viwanja vya
Jangwani Jijini Dar es Salaam.
PAPO KWA PAPO Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo
na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia
tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp
+255789925630.
|
No comments:
Post a Comment