KAMPENI CCM 2015:-Wananchi Wamzuia Mgombea Mwenza wa CCM Barabarani Mwanga. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, August 25, 2015

KAMPENI CCM 2015:-Wananchi Wamzuia Mgombea Mwenza wa CCM Barabarani Mwanga.

Bi. Samia Othuman Suluhu akipokewa na baadhi ya viongozi na makada wakiwa kwenye mkutano huo.
BAADHI ya wananchi na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamelazimika kuuzuia msafara wa mgombea mwenza wa nafasi ya urais leo alipokuwa njiani akitokea Wilaya ya Same kuelekea Wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro huku wakimuomba awasalimu na kuzungumza nao, kabla ya kuendelea na safari yake.

Bi. Samia Suluhu alilazimika kuusimamisha msafara wake baada ya wananchi hao kusogea zaidi barabarani wakati akipita huku wakinyoosha mikono ya kumuomba asimame ili azungumze nao eneo la kilometa chache kabla ya kuingia njia panda. Wananchi hao wengi wakiwa wakinamama walimsimamisha kwa kuingia pembezoni mwa barabara alipokuwa akipita na hivyo kulazimika kusimama kwa dakika chache na kuzungumza nao.

Akizungumza aliwaambia amefarijika na kuwaona na mapenzi makubwa na chama chao hivyo kuwaeleza kuwa yeye ni mwanamke pia na anajua kwa karibu kero ambazo wanakabiliana nazo akinamama sehemu mbalimbali na kuahidi endapo watapata ridhaa pamoja na Dk. John Magufuli atahakikisha anasimamia vizuri utaratibu wa kuwawezesha akinamama kupitia vikundi vya kijamii ili waweze kujikwamua kiuchumi pamoja na familia zao.

Alisema yeye ni mwanamke mzazi anatambua shida wanazokumbana nazo akinamama hasa kwenye wodi za wazazi hivyo akifanikiwa kuingia madarakani atahakikisha anasimamia ipasavyo ilani ya chama ambayo imeeleza vizuri juu ya uboreshaji huduma za afya ikiwemo wodi za akinamama na hali ya upatikanaji madawa......BOFYA HAPA KWA TAARIFA ZAIDI.

PAPO KWA PAPO Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.  

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad