![]() |
|
Mgombea
wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk.John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi Mishamo
mkoani Katavi . Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk John Magufuli amesema akiingia madarakani mawaziri wazembe hawatakuwa na nafasi. Akizungumza mkoani Katavi jana August 24,2015, Magufuli alisema iwapo atachaguliwa kuwa rais baada ya uchaguzi mkuu mwaka huu atateua Baraza la Mawaziri la wachapa kazi na atakayeshindwa kwenda na kasi yake atamfukuza. Pia, alisema ataunda baraza dogo la mawaziri ili fedha nyingine itumike kutatua kero za Watanzania na kwamba wala rushwa na mafisadi watachukuliwa hatua ikiwa pamoja na kufungwa ili wananchi waishi kwa raha. Dk. Magufuli alitoa kauli hiyo jana wakati wa mikutano yake ya kampeni yenye lengo la kuomba kura kwa wananchi katika uchaguzi unatarajia kufanyika Oktoba 25, mwaka huu 2015 na kwamba mawaziri wake lazima wawe wachapakazi ili kutatua shida za Watanzania. Alisema anatambua shida za Watanzania kwani amepita katika maeneo mbalimbali na kutambua mahitaji ya wananchi na hivyo baraza lake la mawaziri lazima liwajibike kutatua shida hizo....BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI. |
![]() |
| Wananchi wa Mishamo wakimsikiliza Dk.John Pombe Magufuli kwenye mkutano wa kampeni za CCM mkoani Katavi. |
![]() |









No comments:
Post a Comment