TASWIRA PICHA:-Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia CHADEMA, Mh. Lowassa na kupanda Daladala katika ziara yake eneo la Gongo la Mboto jijini Dar. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, August 24, 2015

TASWIRA PICHA:-Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia CHADEMA, Mh. Lowassa na kupanda Daladala katika ziara yake eneo la Gongo la Mboto jijini Dar.

Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akisalimiana na kushangiliwa na wananchi aliokutana nao katika Kituo cha Mabasi cha Gongo la Mboto mwisho, Jijini Dar es salaam leo August 24, 2015, wakati alipofanya ziara ya kushtukiza eneo hilo ili kujionea hali halishi ya biashara ndogo ndogo. 

Mh. Lowassa aliianza ziara yake eneo hilo la Gongo la Mboto na baadae alipanda daladala mpaka Pugu Kajiungeni, jijini Dar es Salaam.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.

Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Bi. Kulwa Juma ambaye ni mfanyabiashara ndogo ndogo ya kuuza Mihogo ya Kukaanga katika Kituo cha Mabasi cha Gongo la Mboto mwisho, Jijini Dar es salaam leo August 24, 2015, wakati alipofanya ziara ya kushtukiza eneo hilo ili kujionea hali halishi ya biashara ndogo ndogo.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akimsikiliza Bi. Kulwa Juma ambaye ni mfanyabiashara ndogo ndogo ya kuuza Mihogo ya Kukaanga katika Kituo cha Mabasi cha Gongo la Mboto mwisho, Jijini Dar es salaam leo August 24, 2015.

Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akizungumza na vijana wanaoendesha Bodaboda waliokuwepo kando ya Kituo cha Mabasi cha Gongo la Mboto mwisho, Jijini Dar es salaam leo. Kulia ni Mgombea Mweza wake, Dkt. Juma Haji Duni.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akiwa katikati ya umati wa watu wakati alipotembelea eneo la Gongo la Mboto mwisho, Jijini Dar es salaam leo August 24, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akizungumza na baadhi ya wanafunzi waliokuwa kituoni hapo kusubiria usafiri.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akiwa ndani ya Daladala alilopanda kutokea Gongo la Mboto Mwisho mpaka Pugu Kajiungeni jijini Dar es salaam,mapema leo August 24, 2015 asubuhi.
Mh. Lowassa akishuka kwenye daladala.
Wakazi wa mji wa Mbagala wakiushangilia msafara wa Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa pamoja na Mgombea Mweza wake, Dkt. Juma Haji Duni wakati walipotembelea Kituo cha Mabasi cha Mbagala Rangi tatu jijini Dar es salaam, wakati walipotembelea kituo hicho leo August 24, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akizungumza na Vijana wanaojihusisha na shughuli mbali mbali katika stendi kuu ya Mabasi yaendayo mikoa ya Lindi na Mtwara, ilipo Mbagala jijini Dar.
Mgombea Mwenza wa Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Juma Haji Duni akiwasalimia wakazi wa Mbagala.
PAPO KWA PAPO Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp  +255789925630.  

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad