EPL 2015 / 2016:- Taswira Picha Swansea 2-1 Manchester United leo August 30,2015. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, August 30, 2015

EPL 2015 / 2016:- Taswira Picha Swansea 2-1 Manchester United leo August 30,2015.

Golkipa Romero wa Manchester United akiwa chini baada ya kukubali leo hii August 30,2015 kufungwa na  Swansea City wakitoka nyuma kwa Bao 1 na kuifunga Manchester United Bao 2-1 na kuwapa kipigo chao cha kwanza kwenye Ligi Kuu Uingereza kwa Msimu huu mpya 2015/2016.
Hadi Mapumziko, Mechi hii iliyochezwa huko Liberty Stadium, ilikuwa 0-0.

Dakika 3 tu baada ya Kipindi cha Pili kuanza Juan Mata aliipa Man United Bao ikiwa ni zawadi kwa kuitawala Mechi hii yote.

Hadi Daki ya 60 Man United walionekana ni washindi lakini Dakika 1 baadae Mchezaji wa Kimataifa wa Ghana, Andre Ayew, akaisawazishia Swansea na Dakika 5 baadae, Mtu wao hatari, Bafetimbi Gomis akawapa Bao la Pili na la ushindi.

 Ligi Kuu Uingereza sasa inasimama kupisha Mechi za Kimataifa na itarejea tena Septemba 12,2015  na Man United wapo kwao Old Trafford kupambana na Mahasimu wao wa Jadi Liverpool ambao Jana August 28,2015 wakiwa kwao Anfield walinyukwa 3-0 na West Ham.

Jumamosi Septemba 12,2015

1445 Everton v Chelsea    
     
1700 Arsenal v Stoke 
            
1700 Crystal Palace v Man City     
           
1700 Norwich v Bournemouth    
              
1700 Watford v Swansea      
          
1700 West Brom v Southampton   
           
1930 Man United v Liverpool   
       
Jumapili Septemba 13,2015.

1530 Sunderland v Tottenham  
                
1800 Leicester v Aston Villa  
          
Jumatatu Septemba 14,2015.

2200 West Ham v Newcastle

PAPO KWA PAPO Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad