Katika sensa iliyofanyika hapo awali
ilibainika kuwa mkoa wa Kagera una jumla ya kaya 509,710 ambazo zitagawiwa
jumla ya vyandarua 1,810,250 ambapo kaya moja inaweza kupata zaidi ya chandarua
moja kwa kutegemea wanankaya waliopo na walioandikishwa wakati wa sensa.
Mratibu wa Malaria Mkoani Kagera Dk. Julian Mugengi akisoma taarifa katika
uzinduzi huo alisema kuwa Mkoa wa Kagera umekuwa na historia ya milipuko ya
malaria hasa katika Wilaya ya Muleba kwa miaka ya 1997, 1998, 2007, na mwaka
2013.
Dk. Juliani alisema kuwa katika
taarifa ya utafiti wa viashiria vya UKIMWI na Malaria ya mwaka 2007 ilionyesha
kuwa mkoa wa Kagera ulikuwa na maambukizi ya malaria kwa asilimia 42% hadi 50%
na mwaka 2010 kiwango hicho kilishuka hadi asilimia 10% hiyo ilitokana na
mabadiliko ya hali ya hewa.
Kwa mwaka 2015 wagonjwa waliopima
katika vituo vya kutolea huduma maambukizi ya malaria yalikuwa juu kwa miezi ya
Januari na Februari kwa watoto juu ya miaka 5, na watoto chini ya miaka 5
maambukizi yalikuwa asilimia 59.1%.
Aidha maambukizi ya vimelea vya malaria
yalipungua kwa mwezi Marchi hadi Juni 2015 kutokana na unyunyiziaji wadawa ya
ukoko majumbani uliofanyika katika Wilaya za Biharamulo Ngara na Muleba na
kupunguza mambukizi hadi Julai 2015 watoto chini ya miaka 5 yalikuwa asilimia
25.7% na wakubwa asilimia 4.6% kwa wagonjwa waliopima katika vituo vya kutolea
huduma.
Kauli mbiu ya mwaka huu 2015 inasema
“Wekeza kwa Maisha ya Baadae, Tokomeza Malaria”
PAPO KWA PAPO Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo
na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia
tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp
+255789925630.
|
Friday, August 14, 2015
Home
HABARI
MALARIA HAIKUBARIKI:-Viongozi wa serikali za Mitaa Kagera waonywa kutochakachua Ugawaji wa Vyandarua vya bure.
MALARIA HAIKUBARIKI:-Viongozi wa serikali za Mitaa Kagera waonywa kutochakachua Ugawaji wa Vyandarua vya bure.
Tags
# HABARI
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
HABARI
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment