Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akipongeza na baadhi
ya Wagombea Udiwaki wa Kata mbali mbali za Mji wa Makambako, Mkoani Njombe
baada ya kuhutubia Mkutano wake wa Kampeni.
Mgombea
urais wa vyama vinavyounda UKAWA Mh Edward Lowassa ameendelea kunadi sera zilizoko
kwenye ilani ya umoja wa vyama vyao katika wilaya za mkoa wa Njombe huku
wananchi, viongozi, na wagombea wa UKAWA wakiwataka watanzania kutambua kuwa
hatua ya wagombea wa CCM ya kuendelea kulalamika na kutoa ahadi ni kielelezo
cha kutosha kuonyesha kuwa hawana jipya
na wamepoteza sifa za kuongoza.
Pia Mh.Lowassa alieleza sera zilizoko kwenye
ilani ya UKAWA na namna alivyojipanga kuwatumikia watanzania kama wakimchagua
kuwa rais likiwemo la kuondoa tabaka la maskini na tajiri sambamba na
kuwahakikishia watanzania suala la amani.
Waliowahi
kuwa mawaziri mkuu wa serikali ya CCM, Mh Fredrick Sumaye na Waziri wa mambo ya
ndani ,Laurence Masha ambao wamehamia UKAWA wakaendelea kuweka wazi umuhimu wa
watanzania kupokea mabadiliko.
Baadhi ya
wananchi wamesema baada ya kusikia sera za UKAWA wana matumaini makubwa ya
kuondokana na matatizo waliyonayo chini ya Mh Edward Lowassa ambaye wanajua
utendaji wake.
Habari na
:-ITV.
|
Tuesday, September 01, 2015
Home
SIASA
KAMPENI UKAWA 2015:-Taswira ya Mkutano wa Mh. Edward Lowassa Mkoani Njombe August 31,2015 na na namna alivyojipanga kuwatumikia Wwatanzania.
KAMPENI UKAWA 2015:-Taswira ya Mkutano wa Mh. Edward Lowassa Mkoani Njombe August 31,2015 na na namna alivyojipanga kuwatumikia Wwatanzania.
Tags
# SIASA
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
SIASA
Labels:
SIASA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment