UP DATE YA AJALI YA BASI NA TRENI TABORA:- Yaua wa Nne Papo Hapo leo July 27,2015. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, July 27, 2015

UP DATE YA AJALI YA BASI NA TRENI TABORA:- Yaua wa Nne Papo Hapo leo July 27,2015.

Pichani juu ni muonekano wa Paa la juu la basi  likiwa limeharibika baada ya treni kugongwa na bus la "DONT WORRY" lenye namba za usajili T568 ABP huko eneo la Malolo nje kidogo ya mji wa Tabora mkoani Tabora leo Julai 27,2015 ambapo  Mashuhuda wa ajali  hiyo  wamesema kuwa, dereva aliyekuwa katika mwendo wa kasi alitaka kukatiza haraka bila kuzingatia eneo hilo inapopita Treini hata kama aliiona Treini hiyo, na ndipo alipokata kona ya ghafla na basi hilo kuanguka kwenye reli na Treini kuigonga na kukutoa paa lote la juu la gari.

Watu wanne wamefariki papo hapo na wengine zaidi ya 40  kujeruhiwa baada ya Treini ya mizigo,kuligonga basi kampuni ya Don’t Worry lililokuwa likitokea mjini Tabora kuelekea Ufuruma  wilayani Uyui mkoani Tabora leo July 27, 2015 na  lilipofika eneo la kivuko cha reli eneo la Malolo manispaa ya Tabora katika kile kilichodaiwa kuwa ni uzembe wa dereva.

Aidha kaimu kamanda wa polisi mkoani Tabora ,Kamishina msaidizi Juma Bwire amesema kuwa katika ajali hiyo ya basi lenye namba za usajili T568 ABP,wanaume watatu na mwanamke mmoja wamepoteza maisha huku dereva aliyejulikana kwa jina la Kaonjo Iddy (34) akitoroka baada ya kusababisha ajali hiyo ambapo majeruhu wamepelekwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tabora.

Viongozi wa shirika la reli waliofika  katika eneo la ajali hiyo wamesema kuwa madereva hawazingatii usalama wa barabarani kwani shirika la reli limejitahidi kuhakikisha linaweka alama husika lakini kutokana na mazoea mabaya hawajali na matokeo ni kusababisha ajali mbaya kama hiyo.

Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad