|
Alifafanua
kwamba Mradi huo ambao awali ulifadhiliwa na
Benki ya Dunia na kukamilika mwaka 2011, haukuridhiwa kutumika hadi
mwaka jana ulipokuja mradi wa CFIT ambao uliingizia upitiaji upya wa mradi huo
na kuwezesha kuridhiwa kwa matumizi.
Naye kiongozi wa timu iliyopitia awali katika
mradi huo wa CFIT, Profesa Ralph Masenge
amesema wataalamu waliohusika na upitiaji huo kabla ya kongamano walitoka Chuo
cha Ualimu Tabora na kile cha Monduli,Chuo kikuu huria Tanzania na Chuo kikuu cha Dar es salaam.
Alisema
awali walipitia kuona mahitaji maalumu ya walimu kisha wakaja na mapendekezo
ambayo sasa yanafanyiwa kazi .
Alisema
matatizo mengi ya elimu Tanzania yanatokana na uhaba wa vifaa vya elimu na ubora wa walimu.
Alisema
mradi huo utasaidia kutoa elimu bora kwa kuwa na walimu bora na vifaa bora
kupitia Tehama.
Alisema
mradi huo utasaidia kuwezesha Tehama
kutumiwa kama chombo cha kutumia wanafunzi hasa pale panapokosekana.
Profesa
Masenge alisema hatua waliyofikia ni hatua ya matayarisho na kwamba ni
matarajio yao kwamba wakishafikisha hati
hiyo kwa wizara masuala ya matumizi ya maabara yatakuwa yamekamilika.
|
No comments:
Post a Comment