PICHA / AJALI YA BASI KAGERA:-Watu wanne wafariki dunia baada ya Basi la Sabuni Express kugongana uso kwa uso na Gari ndogo Toyota Land Cruiser leo July 28,2015 eneo la Bugorora. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, July 28, 2015

PICHA / AJALI YA BASI KAGERA:-Watu wanne wafariki dunia baada ya Basi la Sabuni Express kugongana uso kwa uso na Gari ndogo Toyota Land Cruiser leo July 28,2015 eneo la Bugorora.

Pichani juu na chini ni Muonekano wa  magari , Basi la Kampuni ya Sabuni Express lenye namba za Usajili T 950 BFW linalofanya safari zake kati ya wilaya ya Karagwe mkoani Kagera na Jiji la Mwanza kugongana uso kwa uso na Gari ndogo aina ya Toyota Land Cruiser namba T 169 AJU mali ya Kanisa Katoliki Jimbo la Rulenge Ngara, katika ajali  iliyotokea leo July 28, 2015 Majira ya saa mbili Asubuhi,eneo la Kijiji cha Kagare, kata ya Bugorora wilayani Misenyi Mkoani Kagera na kuua papo hapo Watu wanne ambao ni Mapadre wawili , Sister na Mwanafunzi Mmoja,wote kutoka Jimbo Katoliki la Rulenge Ngara mkoani Kagera .
Akizungumza na Radio Kwizera kutoke eneo la tukio, Paroko wa Parokia ya Ngara Mjini Jimbo Katoliki la Rulenge Ngara, Padre Sixmund Nyabenda amewataja waliofariki kuwa ni Padre Michael Mwelinde, Padre Onesmo Bahabwa  na Sister Magreth Kadede aliyekuwa akifanya kazi Parokia ya Biharamulo na Mwanafunzi mmoja wa Katoke Seminary Evelius Kamugisha na Watu wengine 10 kujeruhiwa.

Aidha amesema  Mapadre hao walikuwa wakifundisha katika Shule ya Seminary ya Katoke wilayani Biharamulo na walikuwa wakielekea wilayani Karagwe mkoani Kagera kwenye Misa  ya shukrani ya Padre Ekasius Shumbusho aliyepata upadirisho jumapili iliyopita ya July 26, 2015 .

Padre Nyabenda amesema katika ajali hiyo Padre Florian Tuombe na Sr Leticia wamejeruhiwa na kwamba hali zao sio nzuri kwa sasa na walelazwa katika hospitali ya mkoa wa Kagera kwa Matibabu zaidi. 

Aidha Kamanda wa Polisi mkoani Kagera ,Bw.Augustine Ollomi ameiambia Radio Kwizera FM kwa njia ya simu kuwa Uchunguzi wa ajali hiyo unaendelea.
Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad