MSIMU MPYA WA KANDANDA:- Ndani ya DSTV Kutimua vumbi wiki Ijayo. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, July 31, 2015

MSIMU MPYA WA KANDANDA:- Ndani ya DSTV Kutimua vumbi wiki Ijayo.

Meneja Uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Baraka Shelukindo, akijibu maswali ya waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na huduma za DStv. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Multichoice Tanzania, Barbara Kambogi.

Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Multichoice Tanzania, Barbara Kambogi, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa utambulisho wa msimu mpya wa kandanda kwa wateja wa DStv jana jijini Dar es Salaam. 

Kushoto ni Afisa Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu na kulia ni Meneja Mwendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Baraka Shelukindo.(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog).
Afisa Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu, akielezea huduma za kuunganishwa kwa wateja wapya wa DStv, ambapo ving'amuzi pamoja na dishi vinapatikana kwa gharama nafuu kabisa ya Sh.99,000/- kwa mawakala wote wa DStv nchini.

Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Multichoice Tanzania, Barbara Kambogi (wa pili kushoto) akikabidhi zawadi  ya begi kwa mwandishi wa habari, Joseph Michael baada ya kuchezesha droo kwa waandishi waliohudhuria mkutano huo.

 Wanaoshuhudia kushoto ni Afisa Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu na kulia ni Meneja Uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Baraka Shelukindo.

Furaha Samalu na Barbara Kambogi wakikabidhi zawadi ya begi Super Sport kwa mpiga picha wa ITV, Abdallah Kaniki aliyeibuka mshindi katika droo iliyochezeshwa na Multichoice Tanzania wakati wa mkutano na waandishi wa habari. 

Kulia Meneja Uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Baraka Shelukindo.

Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Multichoice Tanzania, Barbara Kambogi akikabidhi zawadi ya T-shirts kwa mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi, Imani Makongoro.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Na Andrew Chale, modewjiblog

Msimu  mpya wa Soka 2015/16,  unatarajia kuanza rasmi Jumapili ijayo kwa kushuhudia ligi mbalimbali Duniani zikichezwa na kurushwa  moja kwa moja kupitia SuperSport   ambayo imejipanga kukuletea  burudani kabambe kwa mashabiki wa soka barani Afrika.

Meneja  uendeshaji wa Multichoice Tanzania , Ronald Baraka Shelukindo mapema jana akizungumza na vyombo vya habari amebainisha kuwa, Wateja wa DStv wakae tayari msimu huu kwenye Ulimwengu wa Mabingwa ambapo  timu mbalimbali zimejiimalisha katika kuakikisha zinatwaa ubingwa.

“Ligi ya mwaka zitakuwa za kasi na kuvutia kwa kila timu. Barcelona wanajiandaa kutawala dunia kwa mara nyingine, huku Manchester United wanahitaji kurudisha  kiti chao cha Ubingwa Uingereza. 

Jose Mourinho  analenga kuhakikisha Chelsea inabaki  juu,  wakati huo huo , Hispania inajiandaa kuhakikisha wanashinda kwa mara ya tatu kombe la Euro 2016.” Ameeleza Baraka Shelukindo.

 Ameogeza kuwa, Watazamaji wa SuperSport  watakuwa na  nafasi ya kipekee kushuhudia mechi  kwenye ubora wa  HD, ikiwa ni pamoja na michuano ya  Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) , Ligi ya Hispania (La Liga) , Ligi ya Mabingwa wa Ulaya(UEFA) na Ligi ndogo ya Ulaya ( Europa) ,mechi  za FIFA za kirafiki za kimataifa na Klabu Bingwa ya Dunia , Kombe la Ujerumani ,  Kombe la Mfalme  Hispania (Copa Del Rey) , Kombe la  FA na zaidi.

Kwa upande wake, Meneja  Uhusiano wa Multichoice Tanzania, Barbara Kambogi anaeleza kuwa, Katika msimu huu , Ulimwengu wa Mabingwa itakuwa ikionyesha mechi zaidi ya 900 za kimataifa. 

Wateja wa DStv Compact Plus wataweza kufurahia baadhi ya mechi zaidi ya 450 ‘live’, huku Wateja wa  DStv Premium watazawadiwa  mechi zote ‘Live’ zitakazorushwa katika chaneli zote za SuperSport .

 “Kuanzia msimu huu na kuendelea,  vituko vyote vya Ligi Kuu ya Uingereza  vitakuwa  vikiletwa kwenu kupitia SuperSport 5 ( SS5 ) inayopatikana kwenye kifurushi cha Premium. 

 SS5 sasa itakuwa ni nyumba ya soka la Afrika kwa ligi kuu ya Uingereza  huku ikijumuisha  mechi  3 ‘Live’ kila Jumamosi na Jumapili.  Kuambatana na mechi  kutakuwa na vipindi maalum vya soka  kama  PLTV Kick Off, Match Day Live, Fan Zone, Saturday/Sunday Review, Football Today, Classic Matches, Netbusters na  Mech za Wiki” Amebainisha Barbara Kambogi.

Moto wa  La Liga utawashwa  ndani ya SuperSport 3 ( SS3 ). Chaneli hii itakuwa inakuletea  mechi hadi tatu za ligi ya Hispania ‘ Live’ kwa siku ya Jumamosi na Jumapili .  

Wateja wa DStv Premium na Compact Plus  watapata nafasi ya kuangalia  mechi za michuano ya Kombe la mashindano Uingereza ndani ya SS3 sambamba na  mechi za Jumamosi mchana za Ligi kuu ya Uingereza ,  mbadala wa mechi inayorushwa ndani ya SS5,  pamoja na Ratiba zote za  Jumatatu usiku na vipindi vya mahojiano vya studio.

Pamoja na Mechi za ‘Live’ ndani ya  SS3 , itakuwa inakuonyesha vipindi  muhimu  vya shoo za magazeti  , yanayojiri ndani ya  La Liga, pamoja na vipindi maalum  vya ligi za soka . 

Makombe yote ya mpira wa miguu, Mabingwa wa Ulaya na Ligi ya Europa,  Kombe la FA ,  Kombe la Mfalme  Hispania (Copa Del Rey),  Kombe la Ujerumani , Euro 2016 na mechi za kirafiki za kimataifa zitaendelea  kutapatikana kwenye SS3 .

Kwa habari zaidi za michezo na ratiba za mechi kwenye SS5 na SS3, tafadhali tembelea www.supersport.com


Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad