BVR TANZANIA:-Kagera kinara kwa Wageni 708 matatani kwa kujiandikisha BVR. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, July 31, 2015

BVR TANZANIA:-Kagera kinara kwa Wageni 708 matatani kwa kujiandikisha BVR.

Kaimu kamishna wa uhamiaji Tanzania,Bw. Abasi Irovya akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano ofisini kwake jijini Dar es Salaam hapo Jana July 30, 2015, kuhusiana na wahamiaji haramu wanao jiandikisha katika  Daftari la wapiga kura hapa nchini na wale waliojiandikisha zaidi ya mara moja , pia wapo waliokamatwa kutoka Kagera, Mara, Tanga, Kigoma, Dar es Salaam, Rukwa, Kilimanjaro na sehemu zingine.

Kutoka kushoto ni Naibu Kamishna wa uhamiaji wilaya ya Iala, Safina Muhindi,katikati ni Afisa  uhamiaji wilaya ya Temeke, Jaffari Kisesa na Afisa Mdhibiti wa Paspoti, Cripin Ngonyani wakimsikiliza Kaimu kamishina wa uhamiaji Abasi Irovya wakati akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa mikutano ofisini kwao jijini Da es Salaam Jana July 30, 2015.

Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Kaimu kamishna wa uhamiaji Abasi Irovya jijin Dar es Salaam….Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

IDARA ya Uhamiaji nchini imetoa onyo kwa raia wa kigeni watakaobainika kuwa na vitambulisho vya kupigakura baada ya kubaini raia hao zaidi ya 2,000 kuwa na vitambulisho hivyo katika msako unaofanywa na maofisa wao kwenye miji iliyo mipakani hapa nchini.

Idara hiyo imesema tayari imeshaanza kuwachukulia hatua za kisheria raia hao ikiwa ni pamoja na kuwanyang’anya vitambulisho hivyo, kuwaondoa nchini baadhi na wengine kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.

Mikoa ambayo raia hao wamebainika kujiandikisha kwenye daftari hilo na idadi yake kwenye mabano ni pamoja na Kagera (708), Mara (619), Tanga (348), Kigoma (254), Rukwa (13) na Kilimanjaro (12).

Mikoa mingine ni Ruvuma (9), Geita (6), Shinyanga (7), Mtwara (3), Pwani (2), Dar es Salaam (65), Mbeya na Morogoro mmoja kila mkoa. 

Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji nchini, Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Abbas Irovya alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa, maofisa wa Idara hiyo wanaendelea na uchunguzi na watakapowabaini wengine hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Aidha alisema ni kosa kisheria kwa raia yeyote wa kigeni kujiandikisha ili apate kitambulisho cha kupiga kura na hivyo kuwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa kuwafichua raia hao.

Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad