![]() |
| MASWALI
1.
Mnamualika au mnamkaribisha
2.
Vyama vilikuwa vinasema Lowassa ni
dhaifu, leo amekua Imara?
3.
Mnamkaribisha kuingia chama gani
maana UKAWA ina vayama vingi?
4.
Akikubali kujiunga na nyinyi leo hii
mtakubali agombee nafasi ya urais?
5.
Lini mtamtambulisha mgombea wenu
urais?
Lipumba:
Maswali ya ufisadi katika Tanzania ni maswala ya Mfumo, mfumo
wa siasa ndio unaoendeleza ufisadi, Lowassa ameachia madaraka mwaka 2008,
katika kipindi hiki ufisadi umeongezeka au yamepungua? Pia yeye mwenyewe
alisema mwenye ushahidi aende mahakamani.
Swala la kumtangaza mgombea urais ni utaratibu wa vyama,Lakini nina uhakika Mwanzoni mwa mwezi August tutakuwa tumepata mgombea urais ambae atapeperusha bendera ya UKAWA. Kuhusu Lowassa kuepewa nafasi ya kugombea urais: Hilo ni swala la mchakato, mgombea urais atapatika kwa utaratibu ambao upo kikatiba. Mzee Makaidi (NLD) Lowassa ni mtu safi hadi pale atakapobainika mahakamani ni mchafu. Mbatia Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu, kila chama kilichosajiliwa ni mpinzani kwa mwenzake. Watanzania wanahitaji kutengenezewa katiba ambayo itaweka mfumo safi. Mwanzoni wa mwezi wa nane(wiki ijayo) tutamtangaza mgombea wetu kwa mbwembwe, tumeshapiga hatua ambayo ni nzuri. Mbowe: Mazungumzo yameshafanywa hivyo hawezi kuongea na amesema kuhusu picha za Lowassa kuwa kwenye kikao cha CHADEMA zimetengenezwa. Lipumba Kuhusu CUF kusuasua UKAWA: Chama chetu hakijasusua bali kilikuwa kinafuata taratibu za chama na mkutano mkuu umebariki, yeyote atakaechaguliwa kupitia UKAWA, mimi nitamuunga mkono, chama kimebariki maamuzi haya, unapozungumza na mwenyekiti wa CUF basi ndio unazungumza na CUF.ZAIDI BOFYA HAPA KUSOMA |
Monday, July 27, 2015
Home
SIASA
MBIO ZA URAISI TANZANIA 2015:-Yaliyojiri Mkutano wa UKAWA na Wahariri, Makao Makuu ya CUF Leo July 27,2015.
MBIO ZA URAISI TANZANIA 2015:-Yaliyojiri Mkutano wa UKAWA na Wahariri, Makao Makuu ya CUF Leo July 27,2015.
Tags
# SIASA
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
SIASA
Labels:
SIASA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.







No comments:
Post a Comment