MATUKIO YA PICHA:-Ni wakati Wazee wa Kimila wakimkabidhi Katibu Mku wa CHADEMA Dkt. Willibroad Uchifu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, July 05, 2015

MATUKIO YA PICHA:-Ni wakati Wazee wa Kimila wakimkabidhi Katibu Mku wa CHADEMA Dkt. Willibroad Uchifu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani.


Wazee wa Kimila Ali Mahita Mwinyikambi (kulia) na Athumani Rajab Uloleulole kwa niaba ya Wazee wa Pwani wakimtazama Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Willibroad Slaa baada ya kumvisha nguo za kimila na kumkabidhi silaha za jadi ikiwa ni ishara ya kumtawaza kuwa Chifu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani na kumpatia jina la Chifu Mwinyikambi  hapo Jana Julai 04,2015.




Mzee Mwinyijuma Said Muhigira akimkabidhi Katibu Mku wa CHADEMA Dkt. Willibroad Saa usinga, mundu na shoka ikiwa ni ishara ya kumkabidhi Uchifu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani, ambapo Wazee wa Pwani walimtunuku Dkt. Slaa jina la Chifu Mwinyikambi.


Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willbrod Slaa ametawazwa kuwa chifu wa mkoa na wazee wa Dar es Salaam na kuitaka serikali kuhakikisha inawarudishia wananchi chenji zinazotokana na ufisadi wa Escrow , EPA na Richmond.

Akizungumza katika kongamano hilo la wazee la kutafakari uchaguzi wa mwaka 2015, Dk Slaa alisema ingawa wazee waliungana na Hayati Mwalimu Nyerere kupambana na maadui wa tatu ambao ni ujinga, umaskini na maradhi lakini kwa sasa ameongezeka adui wa nne ambaye ni ufisadi.

“Ujinga alioupinga Mwalimu na wazee umeondoka? Lakini ujinga, umaskini na maradhi na kuna adui wa nne ambaye ni ufisadi,” alisema.

Alisema hakuna Mtanzania ambaye atakwenda dukani na Sh10,000 kununua chumvi na kibiriti halafu akaacha chenji yake dukani kwa makusudi na hivyo Watanzania bado wanadai fedha zao zilizopotea kutokana na ufisadi.

Kadhalika Dk Slaa alisema kitendo cha wazee hao kukutana katika kongamano hilo kinaashiria kuwa wana kiu, njaa na matumaini ya kutaka mabadiliko.

“Mwalimu pia alipokewa na wazee wa Bagamoyo ambao walimuombea dua, akaenda kwenye makaburi na waliunganisha nguvu kumng’oa Mwingereza na kupata uhuru na mimi nawataka wazee wa Dar es Salaam kuongeza nguvu kuing’oa CCM,” alisema Dk Slaa.

Alizungumzia pia uandikishaji wa Daftari la Kudumu la Wapigakura na kuwataka wakazi wa Dar es Salaam kuwa makini na kuhakikisha wanajiandikisha.

Awali, katika kongamano hilo, Naibu Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu na Shura za Maimamu nchini Sheikh Rajab Katimba aliizungumzia kauli ya Katibu wa Itikadi na Uenezi, wa CCM Nape Nnauye ya kuwa CCM itashinda kwenye Uchaguzi Mkuu ujao hata kwa bao la mkono na kusema ni ya kichochezi.

“Wakati nchi inajitahidi kuwa na amani na kuwa na uchaguzi wa haki na huru, kiongozi wa chama anazungumza uchochezi mkubwa ambao kama viongozi wengine wangeusema sidhani kama wangekuwa salama,” alisema.

Sheikh Katimba aliwaasa Ukawa kuwa na umoja na kuwataka wawaite wazee ili wawape ushauri badala ya kulumbana kwani huu si wakati mwafaka wa kuwa na migogoro.


Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad