KAGAME CUP 2015:-Kifahamu Kitita atakacho kibeba Bingwa kwa Mwaka huu 2015. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, July 30, 2015

KAGAME CUP 2015:-Kifahamu Kitita atakacho kibeba Bingwa kwa Mwaka huu 2015.

Michuano imefikia hatua ya nusu fainali baada ya kufanyika robo fainali zenye mvuto.

Nusu Fainali hizi zitakuwa kama marudio ya Mechi za Makundi kwani Timu hizo zilipambana kwenye Makundi yao kwa Azam FC kuifunga KCCA 1-0 kwenye Kundi C na toka Kundi A Gor Mahia kutoka 1-1 na Al Khartoum.

 NUSU FAINALI KAGAME CUP 2015.

Ijumaa Julai 31, 2015 .

Al Khartoum v Gor Mahia  [Mechi Na 27]

KCCA Vs Azam FC [Mechi Na 28]

Jumapili Agosti 2,2015.

MSHINDI WA TATU 

Al Khartoum/Gor Mahia v KCCA/Azam FC

FAINALI KAGAME CUP 2015.

Al Khartoum/Gor Mahia v KCCA/Azam FC

Zaidi ya heshima ya kikombe kinachoshindaniwa kwenye haya mashindano pia kuna donge nono ambalo limewekwa kwa ajili ya Klabu itakayobeba ndoo.

Kama ulikua hujui taarifa ikufikie kwamba bingwa wa Kagame Cup 2015 ataondoka na pesa kiasi cha $10,000 pamoja na kikombe. Tuendelee kufatilia mashidano haya hadi tujue nani ataondoka na kitita hiki.

Heshima ya timu pamoja na pesa hizi zinaweza kwa kiasi kikubwa kusaidi uendeshaji wa klabu na mambo mengine.


Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad