COPA AMERICA 2015:- Taswira Picha wakati Chile wakiibuka Mabingwa jana Julai 04,2015 mbele ya Argentina. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, July 05, 2015

COPA AMERICA 2015:- Taswira Picha wakati Chile wakiibuka Mabingwa jana Julai 04,2015 mbele ya Argentina.

Penati ya Mchezaji Alexis Sanchez imewapa Chile ubingwa wa Copa America 2015 kwa mara ya kwanza kwenye mchezo wa fainali kali na ya kusisimua iliyopigwa usiku wa Jumamosi  Julai 04,2015 kati ya wenyeji Chile dhidi ya Argentina na Chile kunyakuwa kombe hilo kwa penati 4-1.

Kombe hilo linawafanya Chile wamalize ukame wa mataji nchini kwao hasa kwenye mchezo wa soka kwa sababu walikuwa hawajawahi kutwaa taji lolote kubwa la kimataifa kwa  Karne yao ya kushiriki Mashindano bila Taji lolote baada ya kufanikiwa kufika Fainali 4 za Copa America, zile za 1955, 1956, 1979 na 1987, na kufungwa zote.


Ilibidi mikwaju ya penati itumike kuamua Bingwa wa mashindano hayo baada ya kushuhudia dakika 90 za mchezo huo zikimalizika bila timu yoyote kuzifumania nyavu za mpinzani wake. 

Zikaongezwa dakika 30 ambazo pia zilimalizika bila kumpata mbabe wa pambano hilo ndipo mikwaju ya penati ilipotumika kuamua nani ataondoka na mwali huyo aliyekuwa akigombewa na Mataifa ya 12 ya America Kusini.

Matias Fernandez, Arturo Vidal, Charles Arangui na Alexis walifunga mikwaju yao ya penati wakati wachezaji waliokosa penati kwa upande wa Argentina ni Gonzalo Higuain ambaye alipaisha juu wakati golikipa wa Chile Claudio Bravo alipangua mkwaju wa penati uliopigwa na Ever Banega huku Messi akiwa ni mchezaji pekee aliyefunga penati ya Argentina.

Mchezaji nyota wa FC Barcelona Lionel Messi, ameshindwa kutwaa taji kwa mara nyingine kwenye fainali yake ya pili akiwa na Argentina baada ya mwaka jana (2014) kulikosa kombe la dunia mbele ya Ujerumani kwenye fainali za kombe hilo ilizofanyika nchini Brazil.

Messi ameshashinda mataji yote kwenye ngazi klabu, lakini ameshindwa kutwaa taji lolote akiwa ametinga uzi wa Argentina.
Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad