CECAFA KAGAME CUP 2015:-Matokeo ya Mechi za leo July 22, 2015 kwa Yanga SC kushindi huku Gor Mahia na Khartoum wanaendelea kuongoza kundi A. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, July 22, 2015

CECAFA KAGAME CUP 2015:-Matokeo ya Mechi za leo July 22, 2015 kwa Yanga SC kushindi huku Gor Mahia na Khartoum wanaendelea kuongoza kundi A.

Klabu ya soka ya Yanga  SC wamezinduka katika michuano ya Klabu Bingwa ya soka Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama Kombe la Kagame, baada ya jioni ya leo July 22, 2015 kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Telecom ya Djibouti, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

 Yanga SC iliyoanza vibaya mechi za Kundi A kwa kufungwa 2-1 na Gor Mahia ya Kenya, sasa inaweza kwenda Robo Fainali iwapo itashinda mechi zijazo dhidi ya KMKM na Khartoum N ya Sudan.

Mshambuliaji mpya aliyesajiliwa na klabu ya Yanga akitokea Mgambo JKT ya Tanga, Malimi Busungu, leo amefanikiwa kufunga magoli mawili kati ya matatu katika dakika ya 26 kipindi cha kwanza na Dakika ya 68 Busungu alifunga goli la pili kabla ya Mwashiuya hajamalizia bao la tatu na lamwisho dakika ya 74 akipiga shuti kali lililogonga mtambaa panya kisha kumgonga mlinda mlango na kutinga nyavuni. 
Katika mchezo huo ,Amis Tambwe alikosa penati ya kwanza dakika ya 36 baada ya Simon Msuva kuangushwa kwenye eneo la hatari lakini Tambwe alipiga mpira nje.

Dakika ya 45 Yanga ilipata penati baada ya mlini wa Telecom kuunawa mpira kwenye eneo la hatari lakini Simon Msuva mfungaji bora na mchezaji bora wa ligi msimu uliopita penati yake ilipanguiliwa na golikipa wa Telecom Nzokira Jeef.
Beki wa Khartoum N ya Sudan (kushoto), Omer Ali Alkhidr akigombea mpira dhidi ya mshambuliaji wa KMKM ya Zanzibar, Matheo Anthony Simon.

Nao timu ya KHARTOUM N ya Sudan imeionyesha njia ya kurejea Zanzibar KMKM, baada ya kuifunga mabao 2-1 katika mchezo wa Kundi A, Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame.

Mchezo huo uliofanyika mchana wa leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Khartoum ilipata bao lake la kwanza dakika ya saba kupitia kwa Salah Eldin Osman Bilal.

Hilo linakuwa bao la tatu kwa Msudan huyo ambaye sasa analingana na Michael Olunga wa Gor Mahia.
KMKM ilisawazisha bao hilo kupitia kwa Matheo Anthony Simon dakika ya 58 kabla ya Khartoum N kupata bao la pili kupitia kwa Anthony Akumu Agay dakika ya 84.

Kharotum inafikisha pointi sita baada ya mechi mbili, wakati KMKM inabaki na pointi zake tatu ilizovuna kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Telecom ya Djibouti.

Kwa matokeo hayo, Gor Mahia wanaendelea kuongoza kundi A wakiwa na pointi 6, wakifuatiwa na Khartoum ambayo inapointi sita pia lakini wanatofautiana magoli ya kufunga na kufungwa. Yanga wapo nafasi ya tatu wakiwa na pointi tatu sawa na KMKM lakini nao wanatofautihwa kwa maoli na Telecom ndio wanashika mkia kwenye kundi hilo wakiwa hawajapata ponti hata moja.

Al hamisi,Julai 23, 2015.

Hegaan Vs Shandy [Saa 8 Mchana]  
    
APR Vs LLB AFC  [Saa 10 Jioni]

Ijumaa,Julai 24, 2015

Khartoum Vs Gor Mahia [Saa 8 Mchana]     
 
KMKM Vs Yanga [Saa 10 Jioni]

 

 Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad