UCHUMI / BIASHARA:- NMB Kuzindua Huduma ya Master Card. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, June 13, 2015

UCHUMI / BIASHARA:- NMB Kuzindua Huduma ya Master Card.

Meneja wa Usimamizi wa Biashara za kadi (ATM) na Huduma za Ziada, Chihoma Chihoma akizungumza na wanahabari (hawapo pichani)...na hapo akionesha mfano wa MasterCard mpya itakavyokuwa.


Chihoma (katikati) akizungumza na wanahabari.

BENKI ya National Microfinance (NMB) inatarajia kuzindua huduma mpya za mashine ya ATM za MasterCard zijulikanazo kama World Rewards,Titanium na Tanzanite.

Akizungumza leo katika kikao kifupi na wanahabari kwenye Ofisi za GEPF Victoria jijini Dar, meneja wa usimamizi wa biashara za kadi za ATM na huduma za ziada, Chihoma Chihoma, amesema wanatarajia kuzindua huduma hizo za kibenki kutokana na mahitaji ya wateja kuwa juu na kuona vyema kuongeza wigo ili kuwawezesha upatikanaji wa huduma bora na za haraka.

Alisema kuwa huduma hiyo mpya itakapozinduliwa itawawezesha wateja wa NMB kutoa kiasi kikubwa cha fedha kutoka katika ATM za MasterCard tofauti na hivi sasa. Kwenye kadi hizo mpya, mteja ataweza kutumia katika manunuzi ya bidhaa na pia kulipia huduma mbalimbali na mteja anaweza kutoa kiasi cha zaidi ya shilingi milioni moja kila katika ATM tofauti.

Aliongeza kuwa NMB Mastercard ni rahisi kutumika na ni salama kutokana na tekinolojia yake iliyotumika kutengenezea hivyo wateja wakae tayari kupokea huduma hiyo mpya hivi karibuni.

(PICHA/HABARI: DENIS MTIMA/GPL)

Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad