KUOMBA RIDHAA URAIS CCM:-Taswira Picha wakati Wasira alipoingia Bukoba kimya kimya kusaka Wadhamini. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, June 13, 2015

KUOMBA RIDHAA URAIS CCM:-Taswira Picha wakati Wasira alipoingia Bukoba kimya kimya kusaka Wadhamini.

Mbunge Bunda na Waziri wa Chakula na Kilimo,Bw. Stephen Wassira akionyesha fomu baada ya kupata wadhamini 122 mjini Bukoba.....Mwingine ni Mbunge wa Bukoba Vijijini Jasson Rweikiza.
Stephen Wassira akisaini kitabu katika Ofisi za CCM ya Bukoba, Kulia kwake  ni Mwenyekiti wa chama wa Wilaya hiyo Novatus Nkwama.



Wadhamini katika picha pamoja na Stephen Wassira na viongozi wengine.KUONA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

KUTOKA GAZETI LA NIPASHE

Waziri Stephen Wassira ambaye pia ametangaza nia ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema yeye ndiye anayefaa kuwa rais wa nchi kwa sababu anaichukia rushwa na hana kashfa yoyote.

Alisema nchi hii kwa sasa imejaa wala rushwa na kwamba yeye ataikomesha kwa sababu anaichukia wala hajawahi kuiomba au kuipokea, huku akisema kuwa kuna wanachama wenzake, ambao ni wala rushwa wakubwa na kila kashfa wanaguswa lakini sasa wanataka waingie Ikulu kwa kutumia rushwa waliyoivuna wakiwa madarakani.

Aidha, alisema akibahatika kuingia tano bora na kisha tatu bora na badaye akapeperusha bendera ya CCM kama mgombea wa urais kupitia tiketi ya chama hicho, ni lazima viongozi wa Ukawa watajinyonga kwa sababu wanamtambua jinsi alivyo na uwezo.

Ukienda hospitali utakutana na rushwa, polisi rushwa na mahakamani rushwa… Rushwa imeanza zamani maana hata yule aliyekuwa akibeba mikoba ya Yesu, lakini alivyopewa vipande 30 vya fedha akamsaliti Yesu, kwa hiyo rushwa ni tatizo  haikuanza leo, bali ya leo imezidi sana, ipo nyingine ya mikataba mibovu, manunuzi, sasa akiwa Rais ambaye ni mla rushwa atawaonea aibu wenzake.”—Waziri Wassira.

Alisema atahakikisha jembe la mkono kwa wakulima linakuwa historia, ikiwa ni pamoja na kuongeza ajira kwa vijana, kingine ni kuboresha elimu ya sayansi kwa wanafunzi wa sekondari.

Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad