KUFUZU AFCON 2017:- Taifa Stars yafungwa ugenini 3- 0 huku Rwanda ikishinda bao 1-0 dhidi ya Msumbuji. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, June 14, 2015

KUFUZU AFCON 2017:- Taifa Stars yafungwa ugenini 3- 0 huku Rwanda ikishinda bao 1-0 dhidi ya Msumbuji.


Timu ya Taifa ya Tanzania  ‘Taifa Stars’ imeshindwa kutamba mbele ya Mafarao timu ya taifa ya Misri baada ya kukubali kipigo cha goli 3-0 kwenye mchezo wa kuwania kufuzu kucheza fainali za mataifa ya Africa (AFCON) michuano ambayo itafanyika nchini Gabon mwaka 2017.

 Taifa Stars iliweza kuruhusu magoli hayo kipindi cha pili ambapo Rami Rabia aliiandikia Misri bao la kwanza dakika ya 61, lakini dakika nne baadae Taifa Stars iliruhusu goli la pili baada ya Basem Morsi kuifungia Misri goli la pili mnamo dakika ya 65 ya mchezo na dakika ya 70 Mohamed Salah alipachika goli la tatu na kumaliza kabisa mipango ya Taifa Stars kwenye mchezo huo.

Taifa Stars itakuwa na kibarua kigumu kwenye kundi lake kutokana na kupoteza mchezo wake wa kwanza na hali inaonekana kuwa mbaya zaidi kutokana na aina ya timu ambazo imepangwa nazo kwenye kundi moja. Mbali na Misri, Taifa Stars ipo kundi moja na Nigeria pamoja Chad.

Kocha wa Taifa Stars, Mart Nooij ameshinda mechi tatu tu kati ya 17 ambazo ameiongoza Taifa Stars hadi sasa.


Wakati Tanzania imepoteza mechi yake ya kwanza katika kuwania kucheza Kombe hilo, timu zote za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, zimefanya vizuri.

Rwanda ikiwa ugenini chini ya nahodha Haruna Niyonzima imeshinda ugenini kwa bao 1-0 dhidi ya Msumbuji.

Bao hilo moja limeifanya limeiweka Rwanda katika nafasi nzuri ya kufanya vizuri zaidi kuwania kucheza Afcon.

Timu nyingine imefanya vizuri Ethiopia imeshinda kwa mabao 2-1 dhidi ya Lesotho. Kenya nayo ikatoka sare ya bao 1-1 ikiwa ugenini dhidi ya Congo.

Sudan ikiwa nyumbani, imeitwanga Sierra Leone kwa bao 1-0 ikiwa jijini Kharthoum huku DR Congo ikiibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Madagascar.


MATOKEO MENGINE YA LEO JUNE 14, 2015:

Cameroon 1- 0 Mauritania

Gabon 0 - 0 Ivory Coast

Ghana 7 - 1 Mauritius

Togo 2 - 1 Liberia

Equatorial G 1- 1 Benin


Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad