|
Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Issa Bin Shaaban
Simba, enzi za uhai wake.
Habari
zilizofika chumba chetu cha habari mapema asubuhi leo June 15,2015 na kuthibitishwa na
mamlaka husika zinasema Mufti Mkuu wa Tanzania,
Sheikh Issa Bin Shaaban Simba,
amefariki dunia alfajiri ya leo katika hospitali ya TMJ jijini Dar es
Salaam.
Habari hizo
zinasema mwili wa marehemu umeondolewa hospitali hapo na kuhamishiwa hospitali
kuu ya Jeshi ya Lugalo kungoja taratibu za mazishi.
Kwamujibu Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Alhad Mussa Salum amesema kuwa marehemu alikuwa akisumbuliwa na maradhi
ya moyo pamoja na presha.
Mwili wa
marehemu utasafirishwa kesho mkoani Shinyanga
kwaajili ya maziko.
Inna lillahi
wa inna ilayhi raji'un
Ø¥ِÙ†َّا للهِ ÙˆَØ¥ِÙ†َّـا Ø¥ِÙ„َÙŠْÙ‡ِ رَاجِعونَ)
Waziri wa
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa Dkt. Fenella Mukangara (Mb.)
ametuma salamu za rambirambi kwa Baraza Kuu la Waislamu Nchini (BAKWATA) na
Waislamu wote nchini kufuatia kifo cha Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Shaaban
Issa Bin Simba kilichotokea Jumatatu, tarehe Juni 15,2015 katika hospitali ya
TMJ Jijini Dar es Salaam alipokuwa anatibiwa.
Katika
salamu hizo, Mhe. Mukangara amesema kuwa ni jambo la kusikitisha kumpoteza
kiongozi huyo ambaye bado Taifa lilikuwa likimuhitaji hasa katika kipindi hiki
cha kuelekea uchaguzi Mkuu wa mwezi
Oktoba mwaka huu.
Waziri huyo
ameongeza kuwa Mufti atakumbukwa kwa upole
, unyenyekevu wake na kutopenda makuu,wakati wa uhai wake marehemu
alikuwa tayari kumsikiliza kila mtu bila kujali dini au kabila lake.
“Nimepokea
kwa huzuni nyingi taarifa ya kifo cha Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Shaaban
Issa Bin Simba ambaye alikuwa Kiongozi anayeshirikiana vizuri na viongozi wote
wa serikali na vyama mbalimbali katika kuhakikisha Watanzania wanaendelea kuwa
wamoja” amesema .
Amesema
Waziri Mukangara: “Nakutumia salamu zangu za rambirambi wewe Katibu Mkuu,
BAKWATA na waislamu wote nchini na naungana nanyi katika kuomboleza msiba huu
mkubwa katika nchi yetu.
Aidha,
kupitia BAKWATA, natuma salamu za dhati ya moyo wangu kwa familia ya marehemu
kwa kumpoteza mpendwa wao. Napenda wajue kuwa msiba wao ni msiba wangu. Pia,
naungana nao katika kumwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema aiweke pema
peponi roho ya marehemu … Amina.”
Imetolewa
na;
Idara ya
Habari(MAELEZO)
Pata
Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori
inayonifikia wakati wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
No comments:
Post a Comment