KUFUZU AFCON 2017:-Nigeria yapaa Kundini….Taifa Stars usiku huu na Misri. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, June 14, 2015

KUFUZU AFCON 2017:-Nigeria yapaa Kundini….Taifa Stars usiku huu na Misri.

Nigeria imeanzia kileleni mwa Kundi G baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Chad mechi ya ufunguzi kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika 2017 jana uwanja wa Ahmadu Bello,Kaduna.

Shukrani kwao, wafungaji wa mabao hayo, Gbolahan Salami dakika ya 63 na O Ighalo kwa penalti dakika ya 80.   

Mechi nyingine ya Kundi G inazikutanisha wenyeji Misri dhidi ya Tanzania leo mjini Alexandria. 

Katika mechi nyingine za jana June 13, 2015, Algeria iliifumua mabao 4-0 Shelisheli, Mali imeifunga 2-0 Sudan Kusini, Senegal imeifunga 3-1 Burundi na Burkina Faso imeichapa 2-0 Comoro.

Afrika Kusini imelazimishwa sare ya 0-0 na Gambia, Cape Verde imeichapa 7-1 Sao Tome, Angola imeipiga 4-0 Jamhuri ya Afrika ya Kati, Uganda, imeifunga Botswana mabao 2-0, Zambia imelazimishwa sare ya 0-0 Guinea-Bissau na Malawi imefungwa 2-1 na Zimbabwe.

Mechi za juzi June 12, 2015, Tunisia iliifunga mabao 8-1 Djibouti, Morocco ilishinda bao 1-0 dhidi ya Libya na Swaziland walishinda 2-1 dhidi ya Guinea.


Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad