ARSENAL KUBEBA FA YA 12:-Taswira Picha 13 za Mashabiki wake Ngara wafurahia Ushindi kwa sherehe leo June 14, 2015……13 huku timu ya Alexis Sanchez ikifungwa 8 – 7 katika Bonanza la Soka. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, June 14, 2015

ARSENAL KUBEBA FA YA 12:-Taswira Picha 13 za Mashabiki wake Ngara wafurahia Ushindi kwa sherehe leo June 14, 2015……13 huku timu ya Alexis Sanchez ikifungwa 8 – 7 katika Bonanza la Soka.

Pichani Ni Muonekano wa Mashabiki wa Arsenal mjini Ngara ,mkoani Kagera wakiwa wamejipanga mstari Tayari kuanza Sherehe yao ya Pili kwa mwaka huu 2015 kufurahia  moja ya fainali nyepesi kabisa kuwahi kutokea pale Arsenal lipofanikiwa kutetea taji lake la FA 2014/2015 kiulani kabisa baada ya kuifunga Aston Villa 4-0 liyopigwa kwenye uwanja wa Wembley nchini Uingereza.






Katika Hafla hiyo ya leo June 14, 2015,imeanza majira ya saa 10 jioni katika uwanja wa Posta ya Zamani Mjini Ngara kwa mashabiki hao wa Arsenal kujigawa timu mbili ya Alexis Sanchez  na  Per Mertesacker ambapo timu ya Alexis Sanchez  ilikubali kufungwa mabao 8 – 7 na  Per Mertesacker.

WAFUNGAJI  PER MERTESACKER.

Dishoni Bwakunga dk 20

Focas Fotidas dk 35

Moses Chegele dk 44

Paschal Daniel dk 49

Japhet Ruagaze goli 3 dk ya 56,60 na 80

Na Kenes Binagwa dk 88

WAFUNGAJI  ALEXIS SANCHEZ.

Seleman Ally goli 3 dk ya 15,25  na 30

Najimu Zuberi bao 2 dk 50 na 70

Elisante kidenke aka Mzazi goli 2 dk ya 78 na 90.


Usiku huu Mashabiki hao wa Arsenal mjini Ngara wapatao 80 wanafurahi pamoja na mashabiki wenzao wa timu pinzan za Chelsea,Liverpool,Manchester City na Manchester United katika bonge la sherehe kwenye ukumbi wa Muruvyagira hapa mjini Ngara.
UTAKUMBUKA JUMAMOSI YA MAY 30,2015.

Katika fainali hiyo ya FA iliyopigwa kwenye uwanja wa Wembley dhidi ya  Aston Villa ya jijini Birmingham, hadi mapumziko Arsenal walikuwa mbele kwa bao 1-0 lililofungwa na Theo Walcott dakika ya 40.

Kipindi cha pili Arsenal walicharuka zaidi na kupata magoli mengine matatu yaliyofungwa na Alexis Sanchez dakika ya 50, Per Mertesacker dakika ya 62 na Olivier Giroud dakika ya 90.

Ikiwa chini ya Kocha Arsene Wenger, Arsenal iliandika rekodi mpya kwa kutwaa mara ya 12 taji hilo na kuiacha Man United ambayo imetwaa mara 11. 

Rekodi zinaweka wazi kwamba, mara ya mwisho Arsenal kutinga fainali ya Kombe la FA na kufungwa ilikuwa mwaka 2001, wakati ilitwaa taji hili kwa mara ya kwanza mwaka 1930 (kumbuka Simba na Yanga zilikuwa bado hazijaanzishwa).

Aston Villa yenyewe imetwaa ubingwa wa Kombe la FA mara saba huku ikicheza fainali mara kumi na kwa mara ya kwanza ilitwaa ubingwa wa michuano hii mwaka 1887 na mara ya mwisho kucheza fainali ilikuwa mwaka 2000 na ikapoteza.
Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad