WATIA NIA CHADEMA 2015 :-Hii ndio Ratiba ya Uchukuaji Fomu za Kugombea sasa. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, May 11, 2015

WATIA NIA CHADEMA 2015 :-Hii ndio Ratiba ya Uchukuaji Fomu za Kugombea sasa.


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimefungua milango kwa wanachama wake wenye sifa za uongozi kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa kugombea  Udiwani, Ubunge na Urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2015.


Akizungumza na waandishi wa habari Hivi karibuni, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa amesema, mwanachama aliye tayari ajitokeze kuchukua fomu hizo.


Kwa kuzingatia makubaliano ya ushirikiano wao na vyama vinavyounda kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) vya CUF, NCCR-Mageuzi na NLD, ratiba ya CHADEMA imejikita zaidi katika kata na majimbo ambayo hawana wawakilishi.


Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad