Meli kongwe
ya M.V. Liemba, ambayo inatumiwa na UNHCR, kubeba raia wa Burundi kutoka Kijiji
cha Kagunga, mpakani mwa Tanzania na Burundi mpaka Bandari ya Kigoma.
Raia 61 wa
Burundi walioikimbia makazi yao kutokana na Vurugu za Kisiasa yanayoendelea
nchini mwao wamepokelewa katika kituo cha Kasange wilayani Ngara mkoani Kagera.
Mtendaji wa
Kijiji cha Kasange Bw Elias Miduro amesema kasi ya Raia wa Burundi wanaoomba
hifadhi hapa nchini kupitia eneo la Kasange ni kubwa kwa sasa ikilinganishwa na
hapo awali.
Amesema Raia
hao wanaendelea kuhifadhiwa kwenye Kituo hicho na kwamba Shirika la Umoja wa
Mataifa linalowahudumia Wakimbizi, UNHCR limewapa msaada wa Chakula na
Mablanketi huku Shirika la Msalaba Mwekundu likitoa Mahema.
Kwa upande
wake Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Msalaba Mwekundu mkoani Kagera Bw Kagisa
Mtagayo amesema viongozi wa Chama hicho wamefika kwenye Kituo hicho na kubaini
Changamoto zinazowakabili waomba hifadhi hao na kuanza kuwajengea mahema kwa
ajili ya kupata mahali pa kulala.
Source:-Radio Kwizera FM.
Pata
Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori
inayonifikia wakati wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
No comments:
Post a Comment