Akihutubia wawakilishi wa
vikundi hivyo Mei 10,2015, katika ukumbi wa Kajumulo Foundation mjini
Muleba mbunge wa jimbo hilo Profesa Anna Tibaijuka ( Pichani ) amesema vikundi
alivyochangia fedha hizo ni vya wanawake , Vijana pamoja na wazee
Profesa Tibaijuka amesema kuwa
vikundi hivyo ni vile vilivyopata usajili kupitia idara ya ushirika wilayani
humo na kutimiza masharti ya kuanzishwa vikundi vya ujasiliamali hivyo
anaviongezea mitaji viweze kupanuka na kujipatia maendeleo.
Aidha amesema katika ziara yake ya
Mwezi Machi hadi April 2015, kuzungukia wapiga kura alikabidhiwa risala za
vikundi hivyo kwa kutajiwa changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa mitaji, elimu
ya ujasiliamali pamoja na kukosa masoko.
“Wananchama wa vikundi hivyo
hawana budi kuwa wabunifu katika kuendesha vikundi hivyo ambapo halmashauri ya
wilaya iendelee kutafuta fedha kutoka vyanzo vya ndani kusaidia vikundi vya
vijana na wanawake”Alisema Tibaijuka
Viongozi wa vikundi wamepongeza
kuhusu juhudi za mbunge huyo ambaye hakubagua jografia ya jimbo hilo kwani
kahusisha kuchangia vikundi hata vile vilivyoko visiwani ambavyo wajumbe
wake wanaishi mazingira magumu.
Kwa upande wake diwani wa kata ya
Gwanseli (CUF) Julius Rwakyendela amesema kuchangia vikundi hivyo ni wajibu
wake na kwamba alichelewa kuwakumbuka wananchi labda ni kwa nafasi
aliyokuwa nayo ya uwaziri.
Amesema katika kata yake amechangia
kikundi cha vijana wanaotengeneza barabara kwa mikono ambayo alipita na
kushindwa kufikia baadhi ya vijiji kutokana na miundombinu hafifu ya
kuharakisha maendeleo ya kijamii.
Pamoja na hayo Mwenyekiti wa CCM
wilayani Muleba Muhaji Bushako ambaye ametangaza nia ya kuwania ubunge wa jimbo
la Muleba Kusini amebeza uchangiaji wa vikundi akidai ni takrima ya
kutaka kujisafisha kwa wapiga kura.
Bushako amesema kinachofanyika ni
kujinadi kwa kila kijiji kuendelea kuwatumikia wana jimbo lakini muda wake
ameupoteza akiwa Waziri na kufanya zaidi shughuli za kitaifa akiwasahau
wapiga kura aliowawakilisha bungeni. |
No comments:
Post a Comment