VPL 2014/2015:-Yanga SC kukabidhiwa Kombe lake la 25 la Ubingwa wa Ligi Kuu dhidi ya Azam FC leo May 6, 2015..Taifa. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, May 06, 2015

VPL 2014/2015:-Yanga SC kukabidhiwa Kombe lake la 25 la Ubingwa wa Ligi Kuu dhidi ya Azam FC leo May 6, 2015..Taifa.

Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara inatarajiwa kuendelea leo May 6, 2015  kwa mchezo mmoja utakaopigwa katika dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, wenyeji timu ya Azam FC watawakaribisha Mabingwa wapya wa ligi hiyo msimu huu timu ya Young Africans.

Katika mchezo huo timu ya Young Africans itakabidhiwa Kombe lake la 25 la Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara msimu wa 2014/2015, na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dr Fennela Mkangara.
Mchezo huo unatarajiwa kuanza majira ya saa 11 kamili jioni, kwa saa za Afrika Mashariki na kati ili kutoa fursa kwa wadau, wapenzi na mashabiki wa mpira wa miguu nchini kujitokeza kushudia mchezo huo pamoja na shamrashamra za kukabidhiwa kikombe.

Young Africans watakabidhiwa Kombe la Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu huu na mgeni rasmi, huku wadhamini wa ligi hiyo kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom wakimkabidhi zawadi mchezaji bora wa mwezi Aprili Mrisho Ngasa na fedha taslimu sh. millioni moja.


Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad