NUSU FAINALI UEFA 2014/2015:-Taswira Picha 9 Bingwa Mtetezi akipigwa 2-1 na Juventus ..Leo May 6, 2015 ni FC Barcelona v Bayern Munich. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, May 06, 2015

NUSU FAINALI UEFA 2014/2015:-Taswira Picha 9 Bingwa Mtetezi akipigwa 2-1 na Juventus ..Leo May 6, 2015 ni FC Barcelona v Bayern Munich.

Mabingwa watetezi wa soka nchini Italia, Juventus, wakicheza hapo jana usiku Mei 05, 2015 kwao Juventus Arena Jijini Turin Nchini Italia, wameanza vyema Nusu Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI 2014/2015 walipowafunga Mabingwa Watetezi Real Madrid Bao 2-1.


Juventus walipata Bao lao la kwanza Dakika ya 8 kutokana na pasi safi ya Marchisio kumkuta Carlos Tevez ambae Shuti lake lilitemwa na Kipa wa Real Casillas na kumkuta Alvaro Morata aliekwamisha Mpira wavuni huku Real Madrid walisawazisha Dakika ya 27 kwa Bao la Kichwa la Ronaldo kufuatia krosi ya James Rodriguez.

Kipindi cha Pili, Juve walifunga Goli la Pili baada ya kuokoa Kona ya Real na kuanza kaunta ataki kupitia Morata ambae alimpenyezea Tevez alieangushwa na Carvajal na Refa wa Uingereza Martin Atkinson kutoa Penati.

Tevez alifunga Penati hiyo na Juve kutangulia 2-1.


Timu hizi zitarudiana tena Mei 13,2015  huko Jijini Madrid Uwanjani Santiago Bernabeu.

UEFA CHAMPIONZ LIGI 2014/2015 - RATIBA/MATOKEO.

Jumanne Mei 05,2015.

Juventus FC  2 - 1 Real Madrid CF

Jumatano Mei 06,2015.

FC Barcelona v Bayern Munich

Mechi za Marudiano

Jumanne Mei 12,2015.

Bayern Munich v FC Barcelona 

Jumatano Mei 13,2015.

Real Madrid CF v Juventus FC 


Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad