VPL 2014/2015:-Taswira Picha Yanga SC walivyokabidhiwa Kombe la Ubingwa leo May 6, 2015 na Zawadi kutoka FIFA. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, May 06, 2015

VPL 2014/2015:-Taswira Picha Yanga SC walivyokabidhiwa Kombe la Ubingwa leo May 6, 2015 na Zawadi kutoka FIFA.

Wachezaji na viongozi wa Yanga SC wakifurahia Kombe lao la ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kukabidhiwa na Waziri wa Habari wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara jioni ya leo May 06,2015  Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 

Yanga SC walikabidhiwa Kombe hilo baada ya mechi na waliokuwa wanashikilia taji hilo, Azam FC ambayo walifungwa 2-1 na washindi hao wa pili wa msimu huu na kukamata Nafasi ya Pili nyuma yao na hivyo kufuzu kucheza Mashindano ya CAF ya Kombe la Shirikisho Msimu ujao.

Ushindi wa Azam FC umewafanya wafikishe Pointi 48 na Simba SC, wakiwa Nafasi ya 3, wana Pointi 44 huku kila Timu ikibakiza Mechi 1.

Waziri Dk Fenella (katikati) akimkabidhi Nahodha wa Yanga SC, Nadir Haroub 'Cannavaro' cheti kutoka Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA). Kushoto ni Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Yanga SC, Yussuf Manji.
Dk Fenella akimvalisha Medali Nahodha wa Yanga SC, Cannavaro…Ligi Kuu Vodacom itamalizika Jumamosi hii inayokuja.

LIGI KUU VODACOM 2014/2015 -RATIBA

Jumamosi Mei 09,2015.

JKT Ruvu v Simba SC 

Mtibwa Sugar v Coastal Union

Stand United v Ruvu Shooting

Mbeya City v Polisi Moro

Kagera Sugar v Tanzania Prisons

Ndanda FC v Yanga SC

Azam FC v Mgambo JKT
Sherehe za ubingwa baada ya kukabidhiwa Kombe lao ambapo Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu DunianI - FIFA, Joseph Blatter ametuma salamau za pongezi kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF, Jamal Malinzi kufuatia klabu ya Young Africans kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2014/2015.

Katika salamu hizo za Blatter, amemuomba Rais wa TFF kufikisha salamu zake za pongezi kwa klabu ya Young Africans, wanachama, wapenzi wa mpira wa miguu kwa kupata nafasi ya kuiwakilisha nchi mwakani katika michuano ya kimataifa barani Afrika.

Blatter amesema anatambua mafanikio hayo ya kutwaa Ubingwa, yametokana na na jitihada za uongozi, wachezaji, bechi la ufundi, madaktari, wanachama , washabiki na kila mmoja aliyeshiriki katika kufanikisha kutwaa Ubingwa huo.

Mpira wa miguu unapata mafanikio makubwa kwa kuvuka mipaka hadi kuwa kichochezi halisi cha maendeleo, unawasaidia wachezaji wa ngazi zote kuinua vipaji vyao na mbinu katika kuelekezwa na kubadilika wakati huo huo wakiwa wakiwa na nyoyo za ushirikiano.

Aidha Blatter amesema mpira wa miguu kwa sasa ni shule kwa maisha, vijana wa leo wanaweza kufaidika kupitia kucheza mpira wa miguu kwa ngazi ya kijamii na mtu mwneyewe binafsi, ndio maana amewapa salamu za pongezi Young Africans  na kuendeleza kazi yao na kuongoza njia ya mafanikio.

Kujituma kwa klabu ya Young Africans kumewasaidia kushinda Ubingwa huu ikiwa ni ni mara ya 25, huu ni ushindi mkubwa katika mpira wa miguu.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF).


Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad