MAZUNGUMZO:-Hatimaye madereva wa mabasi na malori nchini Tanzania wausitisha mgomo wao. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, May 06, 2015

MAZUNGUMZO:-Hatimaye madereva wa mabasi na malori nchini Tanzania wausitisha mgomo wao.

Hatimaye madereva wa mabasi na malori nchini Tanzania wameamua kusitisha mgomo wao hapo jana May 05,2015  baada ya Serikali kuwahakikishia kuwa inaandaa utaratibu mzuri wa kujibu na kushughulikia matatizo yao.

Mgomo huo ulioanza jumatatu May 04,2015, umesababisha usumbufu mkubwa kwa raia sehemu nyingi nchini Tanzania ambao walikuwa wamejiandaa kusafiri kuelekea katika mikoa mingine jana na leo kwa ajili ya shughuli zao mbalimbali zikiwemo za kibiashara na kijamii.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Bw.Paul Makonda akiwa na viongozi wengine wa Serikali walifika katika kituo cha mabasi yaendao mikoani cha ubungo na kuzungumza na madereva hao wakiwataka wasitishe mgomo wao na kuanza kazi kwani mambo yao Serikali inayafanyia kazi na hivi karibuni watajibiwa.

Kufuatia hali hiyo maderva hao walikubaliana na ombi hilo la Serikali baada ya kutokea kwa Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Freeman Mbowe ambaye naye aliwasihi waache mgomo huo kwani Serikali itafanyia kazi maombi yao.
Mgomo huo ambao ni mwendelezo wa ule uliofanyika Aprili 09, mwaka huu 2015 ,ulipewa uzito na madereva hao baada ya ahadi walizopewa na Serikali kutofanyiwa kazi kama ilivyoahidiwa na Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka.

Hata hivyo, Waziri Mkuu, Bw.Mizengo Pinda ameunda kamati ya iliyotangazwa na Waziri wa Uchukuzi, Bw.Samuel Sitta ya kusimamia usafiri barabarani itakayowakutanisha wadau wote ili kutatua matatizo katika sekta hiyo kila yanapotokea.


Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad