TASWIRA PICHA BURUNDI:-Rais Nkurunzinza ''apinduliwa'' - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, May 13, 2015

TASWIRA PICHA BURUNDI:-Rais Nkurunzinza ''apinduliwa''

Wakaazi wakiamkiambatana na wanajeshi baada ya kusikia taarifa za kumpindua rais Pierre Nkurunziza leo May 13,2015.



Hata hivyo hali bado ni ya kutatanisha, huku Ikulu ya nchi hiyo ikiwa imekanusha kutokea kwa mapinduzi hayo kupitia mtandao wa Twitter, ikisema yameshindwa.

Jenerali Godefroid Niyombare, mkuu wa zamani wa ujasusi nchini humo aliye na ushawishi mkubwa ametangaza mapinduzi hayo saa chache baada ya viongozi wa nchi jirani za Jumuiya ya Afrika Mashariki kukutana jijini Dar es Salaam Tanzania kuzungumzia hali halisi ya Burundi. 

" Rais Nkurunziza ameondolewa madarakani, serikali imevunjwa, watu wote wanaombwa kuheshimu maisha na mali vya wengine," alisema Jenerali General Niyombare kupitia chombo kimoja cha habari cha kibinafsi nchini humo. 

Kwa sasa takriban watu 20 wameuwawa huku wengine wengi wakijeruhiwa tangu katikati ya mwezi wa Aprili wakati chama tawala cha CNDD FDD kilipomuidhinisha Nkurunziza kama mgombea wao wa Urais katika uchaguzi uliopangwa kufanyika tarehe 26 mwezi Juni 2015.

Mapigano kati ya waandamanaji na vikosi vya usalama nchini humo yamezua wasiwasi kwamba huenda ghasia zikatokea tena katika nchi hiyo ya Afrika ya kati ambayo bado inajikwamua kutoka miaka kumi na mitatu ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyomalizika mwaka wa 2005.

Lakini huku viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC wakitafuta ufumbuzi wa mgogoro wa Burundi raia wa nchi hiyo takriban 50,000 wameripotiwa kuitoroka nchi hiyo na kukimbilia nchi jirani tangu kuanza kwa machafuko. 

Shirika la Umoja wa Mataifa linalowashughulikia wakimbizi UNHCR limesema hali ya wakimbizi inazidi kuwa mbaya na huenda wakimbizi hadi 300,000 wakaihama nchi hiyo...BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI









PICHA NA :-BBC SWAHILI....Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad