EPL 2014/2015:-Liverpool na Gwaride la Heshima kwa Mabingwa Chelsea Jumapili May 10, 2015.! - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, May 04, 2015

EPL 2014/2015:-Liverpool na Gwaride la Heshima kwa Mabingwa Chelsea Jumapili May 10, 2015.!

Liverpool Jumapili May 10, 2015 ,ijayo Uwanjani Stamford Bridge watawajibika kujipanga Mistari miwili kuwakaribisha Mabingwa Wapya wa Uingereza, Chelsea pichani, wakati wakiingia Uwanjani kabla ya Mechi yao ya Ligi Kuu Uingereza.

Gwaride hilo la heshima ni utamaduni wa huko Uingereza wa kuwaheshimu Mabingwa wapya na Mwaka 2007 Chelsea waliwahi kuwaheshimu Manchester United mara tu baada ya kutwaa Ubingwa na Mechi iliyofuata ya Man United kuchezwa Stamford Bridge na Wachezaji wa Chelsea kuweka Gwaride la Heshima [Tazama Picha chini].


Jana Jumapili May 03, 2015 ,Chelsea walitwaa Ubingwa wa Uingereza msimu huu 2014/2015  baada ya kuwachapa Crystal Palace Bao 1-0 ukiwa ni Ubingwa wao wa kwanza tangu 2010 na wa 4 tangu Mrusi Roman Abramovich aanze kuimiliki.

Lakini hili la Kikosi cha Steven Gerrard kuwapigia Makofi Mabingwa wapya Chelsea wakiingia Uwanjani bila shaka litawafurahisha Mashabiki wa Chelsea ingawa Meneja wa Klabu hiyo Jose Mourinho ameuponda utaratibu huo.

Mourinho amesema: "Sipendi hili. Nadhani Spain tuliwahi kufanyiwa mara moja nlipokuwa Real Madrid. Lakini kama ni utamaduni sawa!"
 
Lakini Meneja wa Liverpool, Brendan Rodgers, ambae aliwahi kufanya kazi Chelsea chini ya Mourinho, amesema Chelsea inahitaji heshima.
Alipoulizwa kama Chelsea wanastahili Gwaride la Heshima kutoka Liverpool, Rodgers alijibu: "Wanastahili. Klabu yetu ina misingi ya utu na heshima. Yeyote anaekuwa Bingwa wanamfanyia hilo!"....ZAIDI BOFYA HAPA

Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad