MGOMO WA MADEREVA TANZANIA:- Waziri Mkuu aunda Kamati Kushughulikia Usafiri. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, May 04, 2015

MGOMO WA MADEREVA TANZANIA:- Waziri Mkuu aunda Kamati Kushughulikia Usafiri.

Mabasi ya mikoani yakiwa yameegeshwa katika stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani-Ubungo jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Avila Kakingo,Globu ya Jamii).

Waziri Mkuu Tanzania, Mizengo Peter Pinda.

Waziri Mkuu, Mizengo Peter Pinda ameunda kamati maalumu ya kudumu ya kusimamia Usafiri wa barabarani nchini ili kutatua changamoto zinazoikabali sekta ya Usafiri.

Katika kamati hiyo mwenyekiti wake atakuwa katibu mkuu wa wizara ya chukuzi, Katibu akiwa kamishna wa polisi barabarani na Mkurugenzi wa SUMATRA huku wajumbe wakiwa ni pamoja na katibu mkuu wizara ya kazi ya na ajira, katibu mkuu ujenzi, mwanasheria mkuu wa serikali na naibu katibu mkuu ofisi ya waziri mkuu.

Mkuu wa ratibu wa idara ya maafa toka ofisi ya waziri mkuu, mwenyekiti wa TABOA na TATOA, CHAKUA na wanatakiwa kuanza kufanya vikao leo na kila mwezi watakutana kujadili na kutatua changamoto zote kasoro zile za kisheria ambazo zitapelekwa serikalini kwa mchakato zaidi wa kuzirekebisha.SOMA ZAIDI KWA KUBOFYA HAPA



Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad