VIFO..:-Taswira Picha ya Machimbo ya dhahabu ya Kalole wilayani Kahama yanayodaiwa kuua watu 19 kwa Kufukiwa na Kifusi Baada ya Mvua Kunyesha. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, April 18, 2015

VIFO..:-Taswira Picha ya Machimbo ya dhahabu ya Kalole wilayani Kahama yanayodaiwa kuua watu 19 kwa Kufukiwa na Kifusi Baada ya Mvua Kunyesha.

Wachimbaji Wadogo wakiaangalia sehemu walipofukiwa wenzao wakati wakichimba Dhahabu katika machimbo hayo yaliyoko katika kijiji cha Kalole katika kata ya Lunguya, Halmashauri ya Msalala, ni moja kati ya migodi ya wachimbaji wadogo wanaokisiwa kufikia 30,000 na tayari wengi wao wamejipatia mamilioni ya pesa kwa uchimbaji huo wa kienyeji hali ambao si salama.


Baadhi ya Wachimbaji wadogo katika Mgodi wa Kalole wakihangaika kuwatoa wenzao 19 wanao daiwa kufariki dunia kwa kufukiwa na kifusi ndani ya shimo hilo.


Haya ni baadhi ya Mashimo ambayo wachimbaji wadogo wamekuwa wakichimba katika Mgodi wa Kalole


Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Kalole Bw. Furaha Mashamba akielezea juu ya kutokea kwa tukio hilo la maafa mbele ya Waandishi wa habari hawapo pichani.


Mjiolojia kutoa Ofisi ya Afisa Madini Mkazi Wilayani Kahama Bw. Amir Chande akitoa maelekezo juu ya kufungwa kwa machimbo hayo baada ya maafa hayo kutokea


Wachimbaji wadogo wa Kalole wakifuatilia kwa makini ufukuaji wa wenzao 19 wanaodaiwa kufia ndani ya mashimo walimokuwa wakichimba dhahabu yaliyofunikwa na kifusi kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya kanda ya Ziwa.
Mmoja wa Wachimbaiji katika Mgodi wa Kalole akiwa katika jitihada za kuwafukuwa wenzao wanaodaiwa kufukiwa katika machimbo hayo juzi April 16,2015.
Majeruhi ambaye alisalimika katika tukio hilo akiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kahama akipatiwa Matibabu.

MKOANI SHINYANG’A.

Wachimbaji wadogo 19 wamefukiwa na kifusi wakiwa ndani ya mgodi mdogo wa Kalole kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.

Wachimbaji hao walikuwa wameingia kwenye mashimo nane ambayo baadaye yalibomoka kutokana na kufunikwa na udongo, jambo lililosababisha vifo vyao.

Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Benson Mpesya alisema vijana hao waliingia katika mashimo hayo saa 12:00 jioni kwa lengo la kuiba mawe baada ya muda wa kufanya kazi kumalizika.

Unajua hawa ndugu zetu ni wale wachimbaji wasiokuwa na mashimo ambao muda ukiisha wa kazi huingia kwenye mashimo hayo bila kuangalia usalama na ndivyo ilivyotokea kwa wachimbaji hao,” - alisema Mpesya.

Mpesya alisema kazi ya kufukua maiti hizo lilianza, lakini lilikwama kutokana na hali ya unyevunyevu kwenye mashimo hayo ambayo bado yanaendelea kutitia.

Kati ya maiti 19, saba tayari zimeshatambuliwa na ndugu zao huku nyingine mbili zikiwa bado hazijatambuliwa na tayari tumeomba mashine ya kufukua na ya kunyonya maji kutoka mgodi wa Bulyanhulu ili itusaidie,”- alisema

Hata hivyo, Mpesya alisema idadi hiyo inaweza kuongezeka baada ya kazi ya kufukua kukamilika kwa kuwa hawawezi kujua kama maiti hizo 19 ndio idadi pekee ya watu waliokuwemo ndani ya mashimo hayo.

Tunasubiri wenzetu kutoka mgodi wa Bulyanhulu waje waone kwanza mitambo ipi ambayo inaweza kutumika kuyafukua mashimo hayo kwa kuwa ufukuaji wa kienyeji tuliokuwa tukitumia tumeusimamisha kutokana na mashimo hayo kuendelea kutitia,” - alisema Mpesya.

Machimbo hayo yaliyoko katika kijiji cha Kalole katika kata ya Lunguya Halmashauri ya Msalala, ni moja kati ya migodi ya wachimbaji wadogo wanaokisiwa kufikia 30,000 na tayari wengi wao wamejipatia mamilioni ya pesa kwa uchimbaji huo wa kienyeji hali ambao si salama.

Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

1 comment:

Post Bottom Ad