CAF KOMBE LA SHIRIKISHO:-Yanga SC sasa kazi Ngumu kwa Watunisa baada ya leo April 18, 2015 kutoka Sare. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, April 18, 2015

CAF KOMBE LA SHIRIKISHO:-Yanga SC sasa kazi Ngumu kwa Watunisa baada ya leo April 18, 2015 kutoka Sare.


Vinara na Mabingwa mara 24 wa Ligi kuu soka Tanzania bara Yanga  SC imejiwekea mazingira magumu ya kusonga mbele kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, baada ya kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Etoile du Sahel ya Tunisia jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, ikiwa ni Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 .

Sasa, sare ya kaunzia 2-2 au ushindi wa ugenini kabisa ndiyo utaivusha Yanga SC katika kapu la kuwania kucheza hatua ya makundi ya michuano hiyo, ambako itacheza na moja ya timu zitakazotolewa katika Ligi ya Mabingwa.

Yanga walianza vizuri mno kwa kupata Penati ya Dakika ya Kwanza tu baada ya Kipa wa Etoile du Sahel kumwangusha Simon Msuva na Kepteni Nadir Haroub Cannavaro kufunga Penati hiyo.

Lakini kadri Mechi ilivyoendelea, pengo la Salum Telela lilionekana na Watunisia hao kutawala kabisa Kiungo ingawa hadi Mapumziko Yanga walikuwa mbele 1-0.

Yanga walifanya mabadiliko Kipindi cha Pili kwa kumtoa Kepteni Nadir Haroub 'Cannavaro' alieumia na kumwingiza Salum Makapu.

Etoile du Sahel walisawazisha katika Dakika ya 47 kwa Bao la Mohamed Amine Ben Amor na kuanza staili ya kupoteza muda kulinda Sare yao ya Bao la Ugenini.
Hadii mwisho, Yanga 1 Etoile duSahel 1.

Yanga itarudiana na Etoile du Sahel huko Tunisia Wikiendi ya Mei 5 wakihitaji ushindi au Sare ya kuanzia Bao 2-2 ili kufuzu.


CAF KOMBE LA SHIRIKSHO.

Mechi za Kwanza Raundi ya Mtoano ya Timu 16


RATIBA/MATOKEO.

Ijumaa Aprili 17,2015.

Association Sportive Olympique de Chlef 1 - 1 Club Africain 

Djoliba AC 1 – 2 Hearts of Oak 

Jumamosi Aprili 18,2015.

Young Africans 1 – 1 E.S. Sahel 

Royal Leopards v AS Vita Club

Warri Wolves  v Etanchéité
Jumapili Aprili 19,2015.

CF Mounana v Orlando Pirates

Al Zamalek v Fath Union Sport de Rabat

Onze Createurs v ASEC Mimosas Abidjan

Marudiano Wikiendi ya Mei 5,2015.

Aidha Washindi 8 wa Raundi hii watajumuika na Timu 8 zilizobwagwa nje ya Kombe la Klabu Bingwa na kuwekwa kwenye Droo maalum kupanga Mechi 8 za Mtoano na Washindi wake 8 kutinga hatua ya Makundi ambayo yatakuwa na Makundi mawili ya Timu 4 kila mmoja yatakayocheza Mtindo wa Ligi wa Nyumbani na Ugenini.

 Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad