|
Ripoti imetaja
mikoa 7 yenye maendeleo duni ya watu Tanzania. DODOMA, KIGOMA, SINGIDA, KAGERA,
TABORA, SHINYANGA na PWANI ndio mikoa inayoongoza kwa maisha duni ya watu
Tanzania.
Hayo yamo katika ripoti iliyozinduliwa na
serikali juma lililopita,ripoti hiyo pia imeitaja mikoa inayoongoza kwa hali
bora za maisha ya watu Tanzania kuwa ni: DAR ES SALAAM, ARUSHA, KILIMANJARO,
IRINGA, RUVUMA, MBEYA na TANGA.
Vigezo
vilivyotumika katika utafiti uliozaa ripoti hiyo ni, wastani wa muda wa kuishi
(Life expectancy, max 83.6 - min 20), expected years of schooling, upatikanaji
wa maji safi na salama, umeme, lishe, vifo vya mama wajawazito na watoto,
maendeleo ya jinsia.
Vigezo
vingine ni, mazingira, kipato, umaskini, uhuru na upatikanaji wa mahitaji ya
msingi kama chakula, maji na nyumba.
Utafiti huo
ulifanywa na Economic & Social Research Foundation (ESRF) kwa kushirikiana
na; - National Bureau of Statistics (NBS). - The Office of the Chief Government
Statistician of Zanzibar. - The Department of Economics of the University of
Dar es Salaam na kudhaminiwa na UN.
Source; The Citizen
Pata
Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori
inayonifikia wakati wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
No comments:
Post a Comment