|
"Kabla
ya kampeni kuanza wagombea wakirudisha fomu ndipo mtajua Zitto anagombea jimbo
gani, lakini lazima niongozwe na chama nikagombee wapi , wanaweza kusema Zitto
kagombee jimbo A," alisema.
Aliongeza
kuwa, ACT kinahitaji kujipanga kuingia kwenye mapambano ya kufyeka msitu wa
siasa kwa kuwa ndani yake kuna vyama zaidi 22 na vingine vikiwa na uzoefu
mkubwa kutokana na kudumu zaidi ya miaka 23.
Alisema kazi
kubwa walionayo ni kukijenga chama ili kiweze kulirudisha taifa kwenye misingi
ya waasisi waliyoiacha.
Aliongeza
kuwa, baadhi ya watu wanamuona kama anaanza upya kwa sababu wapo wachache waliwahi
kujaribu na kuishia njiani.
Alipoulizwa
kuhusu wachambuzi wa siasa wanavyomchukulia hivi sasa, Zitto alisema wapo wenye
mtazamo hasi na wengine chanya.
Alisema kwa
wale wanaomchukulia kwa mtazamo hasi anaendelea kuwafundisha na kuwaonyesha
kwamba muono wao ni tofauti wakati wale wa chanya anaendelea kuwasikiliza ili
kupata muongozo zaidi kutoka kwao.
"Tukumbuke
hii nchi watu wamezoea kuchukia mabadiliko angalia kwenye sanaa wakimuona
Diamond amefanikiwa waanza kutoa maneno ambayo siyo, watu wanachukia mabadiliko,"
alisema.
Kuhusu
kuitwa msaliti ndani ya Chadema kwa madai kuwa baada ya kuikosesha Chadema
jimbo kule Katavi, alisema jambo hilo siyo la kweli na kwamba amekitumikia
chama hicho nusu ya maisha yake na alichokifanya kinafahamika kwa wanachama na
viongozi.
"Ambacho
sikufanya mimi ni binadamu sipo sawa kwa kila kitu hakuna binadamu ambaye hana
makosa lakini yapo mema ambayo nimefanya lakini sasa nimeyakunja na kuyaweka
pembeni na tumechora mstari na kuanzisha chama cha siasa cha wazalendo,"
alisema.
Kuhusu
kurasa zake kwenye mitandao ya kijaamii kuwa na maoni hasi, Zitto alisema kila
mtu ana mawazo yake na hawezi kuyabadisha.
"Wito
wangu ni kwa watu ambao ni waoga wa kuchukua maamuzi, waweke akiba ya maneno
kwa sababu ACT ni sawa na moto wa pumba ambao ukiwaka juu unadhani hakuna moto
lakini ukiweka mguu kuna moto mkali sana," alisema.
Source:-allytz.blogspot.com
Pata
Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia
tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
No comments:
Post a Comment