|
Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT -
Tanzania, Zitto Kabwe ameweka hadharani utajiri wake akisema ana fedha taslimu
Sh18 milioni na nyumba mbili zenye thamani ya Sh223 milioni zilizopo Mwandiga,
Kigoma.
Zitto alitangaza mali hizo ikiwa ni sehemu ya kutimiza
matakwa ya katiba na kanuni za maadili ya viongozi wa chama hicho
kinachojinasibu kwa kuenzi sera ya ujamaa wa Hayati Mwalimu Julius Nyerere ya
mwaka 2015.
Kwa mujibu wa fomu hiyo aliyoijaza, Mbunge huyo wa zamani wa
Kigoma Kaskazini (Chadema), hadi Machi 29,2015 alikuwa pia anamiliki fedha katika akaunti
mbalimbali za benki; CRDB ana Sh5.98 milioni, Dola za Marekani 188 (Sh347,000)
na Euro 495 (Sh965,250).
Katika akaunti ya Benki ya NMB anamiliki Sh800,000 wakati katika
Benki ya Stanbic anamiliki akaunti ya familia yenye Dola za Marekani 1,000
(1.85 milioni) akiwa na asilimia 40 na dada yake Thabitha Salumu.
Mbali na
fedha, Zitto anamiliki gari aina Rand Rover Freelander yenye thamani ya Dola za
Marekani 40,000 (Sh74 milioni).
Akizungumzia nyumba alizonazo, Zitto alisema moja ina thamani
ya Sh180 milioni na nyingine Sh43 milioni zote zikiwa mkoani Kigoma.
Source:-mwananchi.co.tz.
Pata
Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila tukio/stori
inayonifikia wakati wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
No comments:
Post a Comment