TEKNOLOJIA:-Taswira Picha 10 za Ndege ya kipekee inayotumia nguvu ya jua ilikwamia China…Ni kitu kimoja tu kimeikwamisha. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, April 20, 2015

TEKNOLOJIA:-Taswira Picha 10 za Ndege ya kipekee inayotumia nguvu ya jua ilikwamia China…Ni kitu kimoja tu kimeikwamisha.

ANGANI.

Ni ndege ambayo ilianza safari yake March 09, 2015 Abu Dhabi na ikafanikisha salama safari zake kwa kupaa angani na kupita Oman, India na Myanmar.

 Marubani wawili wanaoiendesha wanasema wanataka kuvunja rekodi kwa kuuthibitishia ulimwengu kwamba Ndege inayotumia nguvu ya Jua inaweza kutumika kwenye dunia ya sasa.


Pamoja na hayo, safari yao bado ni ndefu ambapo siku mbili zilizopita waliripotiwa na CNN kwamba safari yao imekwama China kwa zaidi ya wiki mbili baada ya kushindwa kupaa kutokana na hali mbaya ya hewa, hali ikiwa mbaya inavunja masharti ya kuipaisha ndege hii.

Jamaa wamepanga kuzunguka na hii ndege kwenye nchi mbalimbali za dunia lakini bila kutumia hata tone moja la mafuta, yani wanataka itumike nguvu ya jua kama ndege ilivyoundiwa.

Picha zote na Millardayo.




 
Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad