TAWIRA PICHA 8:- Ni Treni ya Mwendo Kasi kutoka Dar - Kigoma na Mwanza ikitumia Saa 30 kutua Mwisho wa Reli. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, April 03, 2015

TAWIRA PICHA 8:- Ni Treni ya Mwendo Kasi kutoka Dar - Kigoma na Mwanza ikitumia Saa 30 kutua Mwisho wa Reli.

Treni ya kisasa (Delux), kwenda Bara yenye mabehewa 22 ilianza safari yake ya saa 30 kati ya Dar es Salaam na mikoa ya Kigoma na Mwanza, ikiwa kwenye kituo kikuu cha reli (TRL), jijini Dar es Salaam  Jumatano Aprili 1, 2015.


Treni hiyo iliyopewa jina "Deluxe Coach" imezindua safari yake ya kwanza  Aprili 01, kuelekea mkoani Kigoma, ikiwa na mabehewa mapya yaliyoagizwa na serikali hivi karibuni.

 Injini zilizokarabatiwa na wamalaysia, zimeonekama kama mpya na sasa treni hiyo itakuwa ikisafiri kila Jumapili saa 2 usiku ikitumia masaa 30, ambayo ni pungufu ya masaa 6 yanayotumiwa na treni ile ya kawaida.


Meneja Mkuu Kisamfu, akikagua behewa la daraja la pili kukaa (Second Seat) la Treni hiyo iliyopewa jina "Deluxe Coach" .
Aidha abiria walioanza safari kwa furaha na matumaini April 01, 2015 saa tano asubuhi walitarajiwa kufika Kigoma April 02, 2015 saa 11 jioni badala ya saa tano usiku na  abiria hao watalazimika kuingiza mikono yao zaidi mifukoni, kutokana na kiwango kipya cha nauli kuwa Sh 79,400 badala ya Sh75,700 za awali kwa daraja la kwanza.

Huku nauli za daraja la pili ikishuka kutoka Sh 55,400 hadi Sh,47,600 zile za daraja la tatu zimepanda kutoka Sh 27,700 hadi Sh 35,700.

Abiria wa kwanza wanaoelekea Kigoma, wakifurahia uzuri wa mabehewa hayo.

Treni hiyo itakuwa na madaraja ya tatu , daraja la pili kukaa, daraja la pili kulala, daraja la kwanza na pia patakuwa na hoteli ya kisasa kabisa. treni hiyo mpya inazo huduma za maji kwenye vyumba na vyoo. Meneja mkuu huyo wa TRL ametoa wito kwa watumiaji, kwa kusema neno moja tu "Tukitunze"

Hivi ni viti vya daraja la tatu, ambavyo abiria waliozungumza na wanahabari wamevikosoa kuwa havikuundwa kwa abiria anayesafiri safari ndefu kama ya Dar - Kigoma, bali ni safari fupi , kwani viko wima na hakuna namna yoyote abiria anaweza kujinyoosha kidogo kwa uchovu. "Changamoto" hiyo kwa TRL

Moja ya vyumba vya daraja la pili.

Kwa mujibu wa Meneja Mkuu wa TRL, Kipallo Aman Kisamfu aliwaambia waandishi wa habari kuwa treni hiyo haitakuwa na vituo vingi na kutaja kuwa iking'oa nanga Dar es Salaam, kituo cha kwanza ni Morogoro, na kufuatiwa na Kilosa. Baada ya hapo itasimama kwenye stesheni ambazo ni za miji,wilaya na mkoani.

Sehemu ya kuosha mikono, ambayo iko kwenye korido kwa abiria kunawa

Picha kwa hisani ya K-VIS Blog.


Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad