KATIBA MPYA TANZANIA:-NEC yaahirisha zoezi la upigaji kura ya maoni Aprili 30,2015 sasa Uboreshaji daftari kukamilika Julai. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, April 03, 2015

KATIBA MPYA TANZANIA:-NEC yaahirisha zoezi la upigaji kura ya maoni Aprili 30,2015 sasa Uboreshaji daftari kukamilika Julai.

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Tanzania,Jaji mtaafu Damian Lubuva akitoa tamko.
 
Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Tanzania (NEC) imekubali kuahirisha upigiaji Kura ya Maoni ya Katiba Inayopendekezwa iliyopangwa kufanyika Aprili 30, mwaka huu 2015 kutokana na kutokamilika kwa uandikishaji wa Daftrai la kudumu la wapiga kura kwa kutumia teknolojia ya Biometric Voters Registration (BVR).


Hatua hiyo inakuja baada ya kuwepo mfululizo wa matamko na ushauri kutoka kwa wadau mbalimbali wa demokrasia kwamba zoezi hilo lisingewezekana kwa sasa hasa kutokana kusuasua kwa mwenendo wa BVR.

Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu Damian Lubuva aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Jana April 02, 2015 kuwa kazi ya uboreshaji daftari la wapiga kura ni ya msingi kabla ya taratibu zote za upigaji kura.

Jaji Lubuva aliyeonekana kuwa mpole zaidi, alisema kwa uzoefu walioupata Njombe, zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura bado halijakamilika katika mkoa huo na mingine iliyosalia.
 Hivyo tume haitaweza kuendelea na zoezi la upigaji kura ya maoni na zoezi hilo lililotangazwa hapo awali kufanyika Aprili 30, 2015 limeahirishwa hadi tarehe itakapotangazwa na NEC baada ya kushauriana na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar,” alisema Jaji Lubuva.

Kwa nyakati tofauti, vyama vya siasa, asasi za kiraia, taasisi za kidini na wananchi wamekuwa wakiishauri NEC kuahirisha Kura ya Maoni huku vyama vya siasa vikimtaka Rais Jakaya Kikwete atii makubaliano yaliyofikiwa na Kituo cha Demokrasia (TCD) mwaka jana 2014 ya kuahirisha zoezi hilo hadi baada ya Uchaguzi mkuu wa October 2015.

Jaji Lubuva alisema kuwa tume yake inaendelea kuboresha daftari la wapiga kura nchi nzima ambapo wanatarajia kukamilisha ifikapo Julai mwaka huu. Nec ilieleza kuwa baada ya kumaliza uandikishaji mkoani Njombe watahamia mikoa ya Ruvuma, Lindi, Mtwara na Iringa.


Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila tukio/stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad