![]() |
|
Bi.Zuwena
Abdul (29), Pichani ,Mkazi wa Buzebazeba, Manispaa ya Kigoma Ujiji, ambaye April 01,2015
alijifungua mapacha wanne katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma, Maweni,
anaomba msaada kutoka kwa wasamaria wema, serikali na asasi mbali mbali za
kijamii, ili aweze kuwatunza watoto wake mapacha wanne aliojifungua.
Zuwena
anaomba msaada huo kutokana na kwamba hana kipato chochote kumudu kuwatunza
watoto wake kwani yeye ni mama wa nyumbani na mume wake Rajabu Mkangwa,
anajishughulisha na shughuli ndogo ndogo za uzalishaji.
Ingawa
amesema anajisikia faraja kujifungua mapacha hao, lakini changamoto iliyoko
mbele yake ni namna ya kuwalea kutokana na familia yake kuishi maisha duni.
Mama mzazi
wa Zuwena, Jaqlina Augustino, mkazi wa Gungu Manispaa ya Kigoma Ujiji, amesema
uzazi wa mwanae wa kujifunga mapacha wanne uliwashitua mno, kwani licha ya
familia za pande zote mbili, yaani upande wa Zuwena na ule wa mume wake kuwa na
historia ya mapacha lakini haijawahi kutokea mtu kuzaa mapacha wanne.
Afisa
Muuguzi Msaidizi katika Hospitali ya Maweni, Agnesi Nguvumali, alisema Zuwena
alijifungua kwa njia ya kawaida mapacha wanne jana majira ya saa kumi na mbili
jioni, ambao kati yao watatu ni wa kiume na mmoja wa kike,ambapo amesema kuwa
mtoto wa kwanza amezaliwa akiwa na uzito wa kilo 1.8, wa pili kilo 2.5, wa tatu
1.7na wa nne kilo 1.7.
“Tunawatunza
kwa njia ambayo tunaita Kangaroo, kama ambavyo Kangaroo yule mnyama anavyotunza
mtoto wake kifuani,”alisema Agnesi.
Alisema aina
hiyo ya utunzaji kwa ngozi ya mama na mtoto kugusana, inamsaidia mtoto kupata
uzito mkubwa kwa sababu ya joto la mama tofauti na njia zilizokuwa zikitumiwa
hapo mwanzo ikiwemo ya kuvundika.
“Kikubwa
tunachoomba yule mama kama alivyosema ni mama wa nyumbani, angeweza kusaidiwa
hasa kwenye maziwa ili aweze kutunza hawa watoto wakaweza kukua; kwa yeyote
atakaeguswa aweze kumsaidia huyu mama,”aliongeza afisa muuguzi huyo.
Kaimu Mganga
Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma, Maweni, Fadhili Kibaya,
alisema mpaka sasa hali za watoto hao pamoja na mama yao zinaendelea vizuri.
Kufuatia
kujifungua mapacha hao wanne, Bi. Zuwena sasa amefikisha idadi ya watoto 8
kwani kabla ya mapacha hao yeye na mume wake tayari walikuwa na watoto wengine
4.
Kwa yeyote
mwenye kuguswa na ana nia ya kumsaidia Zuwena Abdul, tafadhali wasiliana nae
kwa namba za simu zifuatazo:- 0759 558472.
Pata
Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori
inayonifikia wakati wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
Friday, April 03, 2015
KUTOA NI MOYO NASI UTAJIRI:-Msaada unahitajika kwa Mama huyu aliyejifungua mapacha 4.
Tags
# HABARI
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
HABARI
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.







No comments:
Post a Comment