TASWIRA PICHA:-Al-Shabab washambulia Chuo Kikuu cha Garissa Kenya. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, April 03, 2015

TASWIRA PICHA:-Al-Shabab washambulia Chuo Kikuu cha Garissa Kenya.


Kifaru cha jeshi la Kenya kikiwasili karibu na chuo kikuu cha Garissa,Garissa, Kenya, April  02, 2015. Aidha Washambulizi wa Al-Shabab wameshambulia chuo kikuu cha Garissa, kaskazini mashariki ya Kenya na kusababisha vifo vya takriban watu 147 kulingana namaafisa wa serikali na zaidi ya 70 kujeruhiwa.


Polisi wa Kenya wakikaribia majengo ya chuo cha Garissa kwa uangalifu mkubwa.


Wananchi wa Garissa wakisubiri kuchangia damu katika hospitali ya Garissa ambako wengi waliojeruhiwa wamelazwa.


Picha juu na chini ni Kifaru cha jeshi la Kenya katika barabara kuelekea chuo cha Garissa, Garissa, Kenya, April 2, 2015.


Wanafunzi wakikusanyika nje ya chuo kikuu cha Garissa kufuatia shambulio la watu wenye silaha, April 2, 2015 ambapo Kundi la al Shabab limedai kuhusika na shambulio hilo.






Maafisa wa polisi wa Kenya wachukua hifadhi nje ya chuo kikuu cha Garissa, April 2, 2015.Picha kwa hisani ya VOA

Kundi la wanamgambo wa Kiislamu wa itikadi kali nchini Somalia la al Shabab ambalo lina mafungamano na kundi la Al Qaeda huko nyuma lilifanya mashambulizi huko Garissa ambayo iko kama kilomita 200 kutoka mpaka wa Somalia na sehemu nyengine za Kenya.

Al Shabab kundi ambalo limehusika na shambulio lililosababisha maafa hapo mwaka 2013 katika jengo la maduka la Westgate katika kitongoji cha kifahari mjini Nairobi limetangaza litaiadhibu Kenya kwa kutuma wanajeshi wake nchini Somalia kwa aili ya kupambana bega kwa bega na wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika dhidi ya kundi hilo.


Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila tukio/stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad