HABARI MBAYA:-Mashabiki Watano wa Simba SC wapata ajali ya gari leo April 3, 2015 mkoani Morogoro. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, April 03, 2015

HABARI MBAYA:-Mashabiki Watano wa Simba SC wapata ajali ya gari leo April 3, 2015 mkoani Morogoro.


Mashabiki na Wanachama wa timu ya soka ya Simba wa tawi la mpira na maendeleo wamepata ajali ya basi i dogo aina ya Toyota Costa Coster lenye namba za usajili T 304 CWL lililopinduka na kuacha njia walilokuwa wakisafiria,mkoani Morogoro wakati wakielekea mkoani Shinyanga  kuisapoti timu yao kwenye mchezo kati ya timu ya Kagera Sugar dhidi ya Simba SC.



Taarifa  za uhakika zinasema watu watano (5) akiwemo kiongozi wa Simba Ukawa, Mohammed Kingolile ‘Ngumi Jiwe’ wamefariki dunia na watu 15 wapo mahututi na wamelazwa katika Hosptali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro wakipatiwa Matibabu.

Ajali hiyo imetokea eneo la Mvomero ikihusisha basi dogo aina ya Toyota Costa lililopinduka na kuacha njia. Polisi bado hawajatoa tamko rasmi.

Waliotangulia mbele ya haki mpaka sasa ni:-,Waluya, Rehema, Ali Kingolile ‘Ngumi Jiwe’ Wabi na dereva wa gari Abdallah Fundi.



Simba SC, mabingwa mara 18 wa Tanzania Bara, watakuwa na kazi ngumu ya kupata pointi dhidi ya kikosi shadidi cha Kagera Sugar katika mechi yao ya kesho usukumani Uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga.

Kagera Sugar FC, mabingwa wa Kombe la Tusker 2004, waliifunga Simba SC bao 1-0 Uwanja wa Taifa jijini hapa Novemba mwaka jana. Shukrani kwa bao la Atupele Green lililokumbusha uchungu wa sare ya 1-1 ya msimu uliopita wa ligi iliyowachefua baadhi ya mashabiki wa Simba SC waliokwaza na refa Mohamed Teofile wa Morogoro baada ya kuipa tuta la dakika za mwisho lililopia sare timu hiyo ya Kagera.

Baada ya kucheza mechi 20, Simba iko nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 32, nane nyuma ya vinara Yanga SC na tano mbele ya Kagera Sugar FC walioko nafasi ya nne baada ya mechi 20 pia.

Mechi 6 za Simba zilizobaki ni:-

Kagera Sugar FC    vs    Simba SC

Simba SC    vs  Mgambo Shooting

Mbeya City FC    vs  Simba SC

Simba SC vs Ndanda FC

Simba SC vs Azam FC

JKT Ruvu vs Simba SC



Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila tukio/stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad