PICHA / AJALI:-Taswira ya Magari matatu kugongana uso kwa uso na kuua Watu 10 mkoani Tanga leo April 9, 2015. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, April 09, 2015

PICHA / AJALI:-Taswira ya Magari matatu kugongana uso kwa uso na kuua Watu 10 mkoani Tanga leo April 9, 2015.


Wananchi wakiwa eneo la tukio.

Watu 10 wamefariki dunia katika ajali iliyohusisha magari matatu katika eneo la Mkata kijiji cha Mbweni wilayani Handeni Mkoani Tanga majira ya saa 5 asubuhi ya leo April 9, 2015.


Kamanda wa kikosi cha usalama barabara mkoa wa Tanga,  Mohammed Mpinga amesema kuwa ajali hiyo imehusisha mabasi mawili ya abiria na gari dogo katika barabara ya Dar es salaa kwenda Tanga na Arusha.

Kwa mujibu wa Kamanda ,gari dogo ilikuwa likitaka kulipita lori lililokuwa mbele yake na ndipo ilipogongana uso kwa uso na basi la RATCO lililokuwa likitokea Tanga kwenda Dar es salaam.

Baada ya basi la RATCO kugonganana na gari dogo, lilipoteza mwelekeo na kugongana tena uso kwa uso na basi la NGORIKA lililokuwa likitokea Dar es salaam kwenda Arusha.

Aidha kamanda huyo amesema kuwa kati ya watu 10 waliofariki dunia ni wanaume watano wakiwemo dereva wa gari dogo na dereva wa basi la NGORIKA pamoja na wanawake watano wakiwemo watoto wawili.

Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi, Amina.
Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad